February 2016 - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Wednesday, February 17, 2016

Mratibu wa matibabu ya Sikoseli katika kitengo ugonjwa huo  kwenye  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Deogratius Soka (katikati) akibadilishana mawazo na wadau. Kushoto ni Promise Mwakale, Ofisa Uhusiano katika taasisi ya sikoseli na kulia ni Dk, Namala Mkopi, daktari bingwa wa watoto na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Watoto (PAT). Imeelezwa Tanzania ni moja ya nchi yenye inadadi kubwa ya wagonjwa wa sikoseli ikikadiriwa kuwa watoto  kati ya 8,000 na 11,000 huzaliwa kila mwaka wakiwa tatizo hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani (wa pili kushoto), ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) akiwa na baadhi ya wadau walihudhuria mkutano   kujadili maendeleo ya tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi cha miaka 10 jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni, Prof. Japhet Killewo, mhadhiri kutoka MUHAS, Dk, Namala Mkopi, daktari bingwa wa watoto na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Watoto (PAT) na Promise Mwakale, Ofisa Uhusiano katika taasisi ya sikoseli.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia) akizungumza na baadhi ya wadau walioshiriki mkutano  kujadili maendeleo ya tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi cha miaka 10 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani akizungumza katika mkutano wa wadau kujadili maendeleo ya tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi cha miaka 10 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Profesa Makani pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS). Sikoseli ni ugonjwa wa kurithi kutoka kwa wazazi wenye vinasaba vya ugonjwa huo.

Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani (kushoto), ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) akiwa na baadhi ya wadau walihudhuria mkutano kujadili maendeleo ya tafiti, elimu, matibabu na mafunzo kuhusu ugonjwa wa sikoseli nchini katika kipindi cha miaka 10 jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Dk. Neema Rusibimayila na Dk Sarah Maongezi mkurugenzi masuala ya afya wa Mfuko wa Wanawake na Maendeleo (WAMA)
Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Benjamin William Mkapa Hiv/Aids Foundation, Hellen Mkondya-Senkoro (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Deloitte,  Zahra Nensi huku Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania (SCFT), Prof. Julie Makani akiangalia wakati wa hafla hiyo. Imeelezwa  ugonjwa wa sikoseli unatibika kirahisi endapo utagundulika mapema katika umri mdogo. (All photos by Peter Mgongo)

Friday, February 12, 2016

Katibu Mkuu wa Chama cha Tenisi Tanzania (TTA),  Bw. William Kallaghe (kulia) akizungumza katika hafla ambayo timu ya taifa ya mchezo wa tenisi ya walemavu (wheelchair tennis) ilikabidhiwa bendera ili kuwaaga kwa ajili ya safari yao kwenda nchini Kenya kushiriki michuano  kadhaa ya kimataifa ya mchezo huo nchini humo. Kushoto ni makamu katibu mkuu wa TTA, Bw. Joshua Mutale na Ofisa Michezo kutoka Baraza la Michezo la Taifa (MBT), Bw. Benson Chacha. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Ofisa Michezo wa  Baraza la Michezo la Taifa (BMT),  Bw. Benson Chacha (kushoto) akizungumza  katika hafla hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa TTA, William Kallaghe na kulia ni ni mmoja wa makocha wa timu hiyo,  Bw.Riziki Salum.
Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bw.Benson Chacha (kushoto),  akikabidhi bendera ya taifa kwa nahodha wa timu ya taifa ya mpira wa tenisi, Juma Mohamed katika hafla yakuwaaga wachezaji hao jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya safari yao kwenda nchini Kenya kushiriki michuano  kadhaa ya kimataifa ya mchezo huo nchini humo.
Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bw.Benson Chacha (kushoto)  akimkabidhi cheti Latifa Nassoro kwa kutambua mchango wa udhamini wa Tanzania Petroleum Service.
Katibu Mkuu wa Chama cha Tenisi Tanzania (TTA), Bw. William Kallaghe (wa pili kulia) akimkabidhi cheti cha shukrani Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bw.Benson Chacha kwa kutambua mchango wa baraza hiko katika maendeleo ya tenisi nchini. wengine pichani ni baadhi ya wachezaji wa timu hiyo. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.(Photos by Brian Peter Mgongo)

Tuesday, February 9, 2016

Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati), akikata utepe kuzindua rasmi kampeni ya  Malengo ya benki hiyo  jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na kulia ni Meneja wa kampeni hiyo, Mtenya Cheya.
Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki ya NBC, Mussa Jallow (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza cha benki hiyo, Andrew Massawe.
Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza cha benki hiyo, Andrew Massawe (kushoto), akizungumza kuhusu faida mbalimbali za mteja wa benki hiyo atakayeshiriki kampeni ya malengo ya NBC. Kulia ni Mkuu wa Huduma za Rejareja za Kibenki wa benki hiyo, Mussa Jallow.
Kampeni ya malengo itadumu kwa muda wa miezi mitatu kutoka Februari 4 mpaka Aprili 30 2016. Katika kipindi hicho cha miezi mitatu ya kampeni,wateja wanaoweka fedha watafaidika na  kiwango cha kuvutia cha riba na kuwa katika nafasi kubwa ya  kushinda gari mpya aina ya Toyota Land Cruiser Prado kama linavooeneka pichani.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya NBC wakipozi kwa picha wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es Salaam. Hii ni kampeni ya tatu ya kuwekeza kuzinduliwa na NBC na kama ilivyo katika miaka mingi kampeni zote zimekuwa za mafanikio makubwa katika suala zima la mrejesho na ufahamu wa wateja. Mwaka jana NBC ilizindua kampeni ya kuwekeza iliyopewa jina la “Weka Upewe” ambayo ilishuhudia NBC ikitoa zawadi kadhaa kwa wateja wao nchini kote.

Tuesday, February 2, 2016

Mkuu wa Mtandao wa Wateja wa NBC Bw. Gaudence Shawa akimkabidhi cheti Bw. Nelson Moshi kwa kuwa mmoja wa wauzaji bora wa NBC kwa mwaka 2015 wakati wa hafla ya Retail Council Awards, iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Wafanyakazi wa NBC idara ya huduma reja reja za kibenki wakisherekea na mwenzao, Evance Luhimbo (Mwenye vazi la Kimasai) kwa kuibuka Meneja Kanda bora wa Mwaka 2015 wakati wa hafla ya Retail Council Awards, iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wengine kwenye picha ni (waliosimama kutoka kushoto) Mkuu wa kitengo cha mikopo, Bw. Andrew Lyimo (kushoto), Mkuu wa Mauzo, Bw. Mongateko Makongoro, Mkuu wa kusimamia hatari za uendeshaji Bw. Arnold Mhally na Mkuu wa Huduma Reja Reja Za Kibenki Bw. Musa Jallow. Wengine kwa mbele ni Bw. Andrew Massawe na Bi Jaqueline Sindano.
Mkuu wa Mtandao wa Wateja wa NBC Bw. Gaudence Shawa akimkabidhi cheti Bw. Methody Tryphone (kulia), kwa kuwa mmoja wa wauzaji bora wa NBC kwa mwaka 2015 wakati wa hafla ya Retail Council Awards, iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kushoto ni Meneja Uendelezaji wa Biashara wa NBC Bw. Eddie Mhina.
Meneja Tawi la NBC Sea Cliff Bi. Mariam Kombo (Kulia) akipokea tuzo ya Meneja Tawi Bora kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Uzingatiaji na Utekelezaji wa sheria za Fedha (compliance and regulatory affairs) wa NBC, Bi.Sarah Laiser-Sumaye, kwenye hafla ya Retail Council Awards, iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Kaimu Mkuu wa Huduma za Digitali na njia za huduma mbadala, wa NBC, Bi. Cynthia Ponera (wa pili kushoto), akipokea Tuzo ya Mkuu wa Huduma Reja Reja za Kibenki kutoka kwa Mkuu wa Idara hiyo Bw. Musa Jallow wakati wa hafla ya Retail Council Awards, iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wengine kwenye picha ni Mkuu wa kitengo cha mikopo, Bw. Andrew Lyimo (kushoto), Mkuu wa Mauzo, Bw. Mongateko Makongoro, Mkuu wa Huduma za Kibenki Binafsi, Bi. Ashura Waziri, na Mkuu wa Usimamizi wa Taarifa, Bi.Tulibako Paiti.
Mkuu wa Idara ya Huduma Reja Reja za Kibenki Bw. Musa Jallow, akimvisha Bw.Robert Kimaro vazi la kimasaai baada kutangazwa kuwa miongoni mwa wauzaji Bora wa mwaka 2015 wakati wa hafla ya Retail Council Awards, iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Wengine kwenye picha ni Meneja Uendelezaji wa Biashara wa NBC Bw. Eddie Mhina na (kushoto) na Mkuu wa Mauzo wa NBC Bw. Mongateko Makongoro.

Pages