Kamanda Ras Makunja mkuu wa kikosi kazi ngoma africa band
Ngoma Africa band aka FFU aka ANUNNAKI ALIEN
Habari
zinaeleza kuwa Ngoma Africa band aka FFU bendi maarufu ya muziki wa dansi
barani Ulaya yenye mako kule Ujerumani inatua nchini Israel kutumbuiza katika
onyesho maalum la siku ya uhuru wa nchi ijulikanayo kama Yom Haatzmaut
siku ya tarehe 1 mpaka 2 Mei 2017 mjini Tel Aviv. Mmoja ya wanaitifaki wa
maonyesho hayo Bi.Shimone amesema bendi hiyo ndio ya kwanza ya kiafrika kupata mwaliko
wa kutumbuiza katika maonyesho hayo lakini hakupenda kuelezea zaidi. Habari za
uhakika zimevuja kuwa bendi hiyo imesafiri kimya kimya kutoka Ujerumani
kuelekea kwa wayahudi kwa ajili ya onyesho hilo. (By Buberwa Jacob)
No comments:
Post a Comment