Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya utengenezaji na uwekaji
wa vifaa vya kuratibu matumizi ya magari na kusaidia upatinakaji wa magari
yaliyoibiwa ya Cartrack Tanzania, Bi. Anna Nyimbo (mwenye jembe), akipiga tuta
la kupandia mbogamboga katika eneo la kijiji cha watoto yatima cha Malaika,
katika hafla ambayo wafanyakazi wa kampuni hiyo walipanda miti ya matunda na
mbogamboga na kisha kukabidhi msaada wa aina mbalimbali za vyakula ikiwa ni
sehemu ya shughuli za kijamii kwa kituo hicho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani jumamosi
iliyopita
Meneja Uendeshaji wa kampuni ya utengenezaji na
uwekaji wa vifaa vya kuratibu matumizi ya magari na kusaidia upatinakaji wa
magari yaliyoibiwa ya Cartrack Tanzania, Bi. Jayne Nyimbo (katikati), akipanda
miti pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha
Malaika Village, katika hafla ambayo wafanyakazi wa kampuni hiyo walipanda miti
ya matunda na mboga mboga na kisha kukabidhi msaada wa aina mbalimbali za
vyakula ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii kwa kituo hicho kilichopo
Mkuranga mkoani Pwani
Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya utengenezaji na uwekaji
wa vifaa vya kuratibu matumizi ya magari na kusaidia upatinakaji wa magari
yaliyoibiwa ya Cartrack Tanzania, Bi. Anna Nyimbo (kulia), akikabidhi msaada wa
aina mbalimbali za vyakula kwa Meneja wa kijiji cha Malaika, James Kalinga
(kushoto), katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanykazi wa Kampuni ya Cartrack wakisaidia
kuandaa shamba kwa ajili ya upandaji wa mbogamboga katika hafla hiyo. Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Cartrack, Albert Mdemu (katikati), akipanda miti pamoja na watoto wanaolelewa katika Kijiji cha watoto yatima cha Malaika, kilichopo Mkuranga, Pwani juzi.
Baadhi ya wafanyakazi
wa Kampuni ya Cartrack wakisaidia kuandaa shamba kabla hawajapanda mbogamboga
ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusaidia jamii.
Watoto wanaolelewa
katika Kijiji cha Malaika wakifurahi pamoja na wafanyakazi wa Cartrack
waliotembelea katika makazi yao na kuwasaidia katika upandaji miti ya matunda
na mbogamboga.
Watoto wanaolelewa katika Kijiji cha Malaika wakila
chakula huku wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Cartrack Tanzania, Anna
Nyimbo (kulia nyuma), walipowatembelea katika makazi yao na kuwasaidia katika
upandaji miti ya matunda na mbogamboga.
Meneja Uendeshaji wa Cartrack Tanzania, Bi. Jayne
Nyimbo (katikati) akiwa na baadhi ya watoto wanaolelewa katika Kijiji cha
Malaika.
Watoto wanaolelewa
katika Kijiji cha Malaika wakiwasindikiza baadhi ya wafanyakazi wa Cartrack
baada ya kuhitimisha ziara yao kituoni hapo. Mkurugenzi Mtendaji wa Cartrack,
Bi. Anna Nyimbo alisema miti ya matunda na mbogamboga walizopanda zitawasaidia
watoto hao katika mahitaji ya kila siku
hivyo kupunguza utegemezi wa misadaa. (All photo by Peter Mgongo)
No comments:
Post a Comment