Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amefunguka na kusema kuwa wao kama viongozi wanazidi kuimarisha huduma mbalimbali za afya ili watu ambao wanamtusi Rais John Pombe Magufuli wazidi kuwa na afya nzuri.
Makonda amesema hayo leo Januari 25, 2018 akiwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam alipokwenda kuzindua jengo la ambalo upasuaji(theater) mbalo litakua na chumba cha na wodi ya wajawazito katika hospitali ya mwananyamala iliyopo wilaya ya kinondoni.
RC Paul akiwa amembeba mtoto mchanga aliezaliwa kwa uparesheni katika hospitali hiyo.
"Wanaoatamba na kumtukana Rais Magufuli ni kwa sababu wazima lakini wakiugua watakuja Mwananyamala, Amana, wengine wataenda Temeke, Muhimbili hata Mlonganzila kuomba matibabu, ila wakiwa wazima waache waseme wanavyotaka, sasa kazi yetu sisi kuwafanya wawe wazima, wakiwa wazima wakija kushukuru sawa na wasipokuja kushukuru basi mwenyezi Mungu anajua namna ya kubariki viongozi wetu wanaofanya kazi zao, lakini mwisho wa siku kubariki Chama Cha Mapinduzi ambacho kimetupatia viongozi waadilifu na waaminifu wanoifanya hii kazi" alisema Makonda
Hili ndilo jengo jipya la upasuaji lililozimduliwa leo ambapo limepewa jina la "PAUL MAKONDA ".
Awali hospitali hio ya mwananyamala ilikua na changamoto nyingi hususa katika upande wa upasuaji kwa wajawazito hali iliyokua inapelekea vifo vya mama na mtoto, lakini jitihada za mkuu wa mkoa Paul makonda kwa kushirikiana na GSM foundation wamewawezesha kukamilisha lengo LA kuwa na jengo lenye vyumba vya upasuaji na wodi za wajawazito ambalo tayar limeshaanza kazi nampaka sasa wajawazito 50 wameweza kufanyiwa upasuaji na wanaendelea vizuri.
Makonda ametoa msisitizo kwa wananchi kuwa na kadi za matibabu ili waweze kupata huduma za afya kwa urahisi pindi wanapokua wagonjwa na pia wawe na tabia ya kupima afya zao mara kwa mara.
"Tiba kwa kadi ni muhimu sana na tutakuja kuzindua kampeni kubwa sana hapa na tutatoa muda fulani kwamba kila mwananchi wa mkoa wa Dar es Salaama lazima awe na kadi yake na kama huna kadi huwezi kupata matibabu, sasa isije kufika hiyo hatua ya kukulazimisha wakati jambo la afya ni muhimu sana" alisisitiza
No comments:
Post a Comment