Waziri wa
Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mh Charles Mwijage (kushoto), akizungumza
na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Mh. Almas
Maige (kulia), huku Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka akisikiliza
wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa
Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa pili kushoto)
akilakiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Almas Maige
(kushoto), na Mratibu wa Mradi wa Mwanamke wa Wakati Ujao, Lilian Machera (kulia) alipokuwa mgeni rasmi
katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho, Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Mama Jayne
Nyimbo (wa pili kushoto), akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi
hiyo wakati wa Mkutano Mkuuu wa Mwaka wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana.
Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka, aliyekuwa
mwenyekiti wa chama hicho, Mhe. Almas Maige na Makamu Mwenyekiti mpya, Felix
Kagisa
Mkurugenzi Mtendaji
wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka (kushoto), akiwa na
baadhi ya maofisa wa chama hicho wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea.
Baadhi ya
washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), wakisikiliza
hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Baadhi ya washiriki katika mkutano huo
wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Charles Mwijage ambaye alisema serikali itaendela kujenga mazingira mazuri ya
utoaji vibali vya uwekezaji ili kuweza kufikia ajenda yake ya kuimarisha uchumi
wa viwanda
Aliyekuwa Mwenyekiti Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Mhe. Almas
Maige akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika pamoja na mkutano kujadili
masuala mbali mbali kuhusu ajira na uwekezaji. (All photos by Mgongos Photography)
No comments:
Post a Comment