Mkuu wa Uhusiano wa Multichoice Tanzania,
Johnson Mshana (Kushoto) akimkabidhi jaketi Balozi maalum wa DStv Mwanariadha
Alphonce Simbu (mwenye fulana ya bluu) wakati wa ziara ya ofisa huyo katika
kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya riadha inayojiandaa kushiriki mashindano
ya riadha ya dunia yatakayofanyika jijini London wiki ijayo. Wa pili kushoto ni
kocha Francis John na kulia ni kocha Anthony Mwingereza. Jumla ya wanariadha 7
wanatarajiwa kushiriki mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia
Marathon. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London.

Balozi maalum wa DStv, Alphonce Simbu (Kushoto)
akiwa na wanariadha wenzake Nelson Mbuya (wa pili kushoto), Stephano Huche na
Joseph Panga(kulia) wakiwa katika
mazoezi makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka mjini Arusha hadi
wilayani Monduli. Wanariadha mbalimbali
wameweka kambi jijini Arusha ikiwemo timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki
mashindano ya riadha ya dunia. Jumla ya wanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki
mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo
yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London.
Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (Kushoto)
akiwa na Wanariadha wenzake Nelson Mbuya (katikati) na Joseph Panga wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa
wiki ambapo walikimbia kutoka mjini Arusha hadi wilayani Monduli.
Mkuu wa Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson
Mshana (Kushoto) akimkabidhi jaketi Balozi maalum wa DStv Mwanariadha Alphonce
Simbu (Kulia) wakati wa ziara ya afisa huyo katika kambi ya mazoezi ya timu ya
taif ya riadha inayojiandaa kushiriki mashindano ya riadha ya Dunia
yatakayofanyika jijini London wiki ijayo. Wa pili kushoto ni kocha Francis John
na mwanariadha Sara Ramadhani. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki
mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo
yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London.

Balozi maalum wa DStv Alphonce Simbu (Kushoto)
akiwa na Wanariadha wenzake wa timu ya taifa itakayoshiriki Mashindano ya
Riadha ya Dunia jijini London wiki ijayo Ezekiel Ng’imba (katikati) na Said
Makula wakiwa katika mazoezi makali mwishoni mwa wiki ambapo walikimbia kutoka
mjini Arusha hadi wilayani Monduli. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki
mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo
yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London.

Mkuu wa Uhusiano wa Multichoice Tanzania,
Johnson Mshana (Kushoto) akimkabidhi jaketi Balozi maalum wa DStv Mwanariadha Alphonce
Simbu (Kulia) wakati wa ziara ya afisa huyo katika kambi ya mazoezi ya timu ya
taifa ya riadha inayojiandaa kushiriki mashindano ya riadha ya Dunia
yatakayofanyika jijini London wiki ijayo. Wa pili kushoto ni kocha Francis John
na mwanariadha Sara Ramadhani. Jumla yawanariadha 7 wanatarajiwa kushiriki
mashindano hayo ambapo watano kati yao wanakimbia Marathon. Mashindano hayo
yanatarajiwa kuanza Agost 4 jijini London. (PHOTOS: Courtesy of DSTV)
Timu ya Riadha yaahidi Medali London!
BALOZI maalum wa DStv na mmoja
wa wanariadha wanaounda timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya riadha ya
Dunia ya mwaka huu yatakayofanyika mwezi ujao jijini London, Uingereza,
Alphonce Simbu, amesema watanzania watarajie medali kutoka kwa timu hiyo kwani
imejiandaa vizuri.
Akizungumza wakati wa ziara
maalum ya Afisa Muandamizi wa DStv, Johnson Mshana katika kambi hiyo iliyopo
Ilboru Arusha ambapo pia alishuhudia mazoezi ya timu hiyo, Simbu alisema kuwa
yeye na wenzake wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha kuwa wanaleta medali
nyumbani katika mashindano hayo makubwa yanayofanyika mapema Mwezi Agosti.
“Tumejiandaa vizuri na
tuna matumaini makubwa ya kushinda. Tumekuwa tukifanya mazoezi mazito na
inaonekana vijana tuko sawasawa kupambana katika mashindano hayo” alisema Simbu
Naye Meneja Uhusiano wa
Multichoice Tanzania, Johnson Mshana ambaye alitembelea kambi hiyo na kisha kushiriki
katika mazoezi amesema kampuni yao imefurahishwa sana na mwenendo wa kambi hiyo
pamoja na timu nzima. “Wakati wote tunapoamua kusaidia katika maandalizi ya
timu tunafahamu fika kuwa timu yoyote bila ya maandalizi ya kutosha haiwezi
kufanya vizuri kwenye mashindano yoyote yale. Hii niyo sababu iliyotusukuma
DStv kusaidia katika juhudi hizi za kuiandaa timu yetu ya Taifa itakayokwenda
kuwakilisha nchi katika mashindano ya dunia. Tunataka Watanzania washuhudie
medali zikija nyumbani”
Amesema baada ya DStv kuanza
kumdhamini Simbu takriban mwaka mmoja uliopita, wameshuhudia mafanikio makubwa
sana. Ambayo yamewatia moyo sana kuamua kuongeza nguvu ili kuiimarisha zaidi
timu ili hatimaye iweze kufanya vizuri zaidi na kuliwakilisha vyema taifa
kwenye michuano ya kimataifa.
“Tulianza na Simbu, amefanya
vizuri, ameshinda, sasa tunaongeza wigo wa ushindi kwa timu yetu ya Tanzania na
tunaamini tutashinda, mbali na hayo DStv ilionyesha mbashara Mumbai Marathon
tukamuona Simbu akishinda, Tukaonyesha Mbashara London Marathon, tukaona Simbu
akivunja rekodi yake, na tutaonyesha mbashara Mashindano ya Dunia Mwezi Agosti,
ambapo bila shaka kwa nguvu hii, tutashuhudia tukikwapua medali kedekede na
kuliletea taifa letu sifa kubwa” alisema Mshana kwa kujiamini.
Naye kocha wa timu hiyo, Francis John amesema, kazi kubwa
imefanywa na makocha wanaoinoa timu hiyo hapo kambini na kwamba
ushirikiano mkubwa kati ya makocha na wachezaji umefanya mazoezi yao kwenda
vizuri. Amesema wanatarajia kuwa wanariadha hao watafanya vizuri kwani
hata mmoja wao aliyekuwa na matatizo ya magoti sasa anaendelea vizuri na bila
shaka atashiriki vizuri kwenye mashindano.
Amesema jumla ya wachezaji saba wakiwemo wanawake watatu na
wanaume wanne watashiriki. Failuna Abdi atashiriki mita 10,000, Gabriel
Gerald mita 5,000 na watano watashiriki marathon kamili ya kilomita 42 ambao
ni Magdalena Krispin, Sarah Ramadhani, Said Makula, Ezekiel Jafar Ng’imba na
Alphonce Felix Simbu.
Timu ya taifa ya riadha itakayoshiriki mashindano hayo inatarajiwa
kuagwa na kukabidhiwa bendera jijini Dar es Salaam tarehe Julai 31 na
Mashindano hayo yanaanza tarehe Agosti 4 2017.
No comments:
Post a Comment