WASTAAFU WA SERIKALI WAMTOA CHOZI RC MAKONDA - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Saturday, January 27, 2018

WASTAAFU WA SERIKALI WAMTOA CHOZI RC MAKONDA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimfariji Bi. Stella Bejumula mstaafu alietapeliwa nyumba yake
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo 
ametembelea na kutoa pole kwa Familia ya Wastaafu ya Bwana Edward Bejumula na Bi. Stella Bejumula walioteseka kwa Miaka Sita bila Makazi baada ya kudhulumiwa Nyumba yao ambapo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kuhakikisha haki inatendeka bila kuvunja sheria.

RC Makonda amewatembelea wastaafu hao na kuwapatia Masada wa vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Unga, Sabuni, Ngano, Mafuta,Nyama,Viazi, Maharage, Sukari, Vitunguu, Ndizi, Nyanya kwaajili ya matumizi ya nyumbani baada ya familia hiyo kupoteza Mali zote. 

Stori ya wastaafu hao kudhulumiwa Nyumba waliyojenga baada ya kufanya kazi kwa Miaka 34 imemgusa RC Makonda hadi kujikuta anashindwa kuvumilia na kutokwa na machozi kutokana na namna inavyouzunisha kuona mnyonge anajituma kwenye kazi na kufanikiwa kujenga nyumba alafu anatokea mtu anatokea mtu anamdhulumu Mali yake.

Makonda amesema kazi ya kutafuta haki  ya wastaafu hao inaanza Mara moja kwa kuwahoji watu wote waliohusika na sakata hilo wakiwemo Benki, Muuzaji wa nyumba, Mnunuzi, kampuni ya udalali ya Majembe, Watu wa Mahakama na watu wa ardhi.

Kwa sasa wastaafu hao wanaishi kwenye nyumba ya mfadhili mmoja aliejitolea kusitiri familia hiyo ambapo RC Makonda amemshukuru kwa moyo alioonyesha. 

Kwa upande wao Wastaafu waliodhulumiwa Mali zao wamefurahia kitendo cha RC Makonda kuona taarifa zao kwenye vyombo vya habari kisha kuwatembelea na kuwasikiliza kitendo kilichowafariji na wanaamini kwa utendajikazi wa RC Makonda wanapata haki yao.

Aidha wamemshukuru RC Makonda kwa kitendo cha kuwapelekea Chakula kwakuwa wameishi maisha ya tabu hadi kukosa vitu vya ndani ikiwemo vyakula ambapo wamemuombea kwa Mungu azidi kumpa maarifa ya kuwasaidia wananchi wanyonge. 
 Bwana Edward Bejumula akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa jinsi walivyotapeliwa nyumba hiyo
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akikabidhi vyakula na mahitaji mbalimbaya kibinadamu alipokwenda kuwatembelea wastaafu hao waliotapeliwa nyumba
Hii ndio  nyumba waliotapeliwa wastaafu hao

No comments:

Post a Comment

SERIKALI YASISITIZA UTAALAMU NA UBUNIFU KATIKA UNUNUZI NA UGAVI

Serikali imewataka wataalam wa ununuzi na ugavi nchini kuongeza ubunifu, uongozi bora na matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuongeza ufani...

Pages