
Mkurugenzi wa Airtel Money, Bw. Andrew Rugamba (wa pili kushoto), akisaini makubaliano (MoU) na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk. Benson Ndiege, ili kuboresha sekta ya kilimo kupitia huduma za mawasiliano na huduma fedha kidijitali. Ushirikiano huu unalenga kuwawezesha wakulima kupata huduma salama na za haraka za malipo, kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kupanua upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu, hususan katika maeneo ya vijijini. Waliosimama wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria wa Airtel Tanzania, Bw. David Lema(kushoto), na Mwanasheria wa TCDC, Bw. Harry Mbogoro. Hafla hiyo ilifanyika mjini Dodoma jana.
Airtel Money Tanzania imesaini makubaliano ya kuingia katika ushirikiano wa kimkakati na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa lengo la kuboresha sekta ya kilimo kupitia huduma za mawasiliano na huduma fedha kidijitali. Ushirikiano huu unalenga kuwawezesha wakulima kupata huduma salama na za haraka za malipo, kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kupanua upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu, hususan katika maeneo ya vijijini.
Akizungumza wakati wa kutangaza ushirikiano huo, Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania, Bw. Andrew Rugamba alisema: “Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), kilimo kinachangia takribani asilimia 30 ya Pato la Taifa na kuajiri zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania. Hata hivyo, bado wakulima wengi wadogo hawajafikiwa na huduma rasmi za kifedha. Kupitia ushirikiano huu, Airtel Money itatoa suluhisho la malipo ya kidijitali kwa wakulima na vyama vya ushirika, kuwezesha ununuzi wa pembejeo, upatikanaji wa simu janja za bei nafuu, pamoja na kujenga historia ya matumizi ya kifedha. Pia tutatoa elimu ya fedha na huduma kwa wateja kupitia mtandao wetu mpana wa mawakala.”
Ushirikiano huu unafikiwa kutokana na mafanikio ya majaribio yaliyofanyika na Airtel kwa kushirikiana na Vyama vya Ushirika vya Masoko ya Mazao (AMCOS), mkoani Morogoro, ambapo Airtel Money lengo lake ni kurahisisha malipo ya pembejeo kidijitali. Matokeo ya awali yalionesha mafanikio makubwa kwa kuongeza uwazi, ufanisi, na upatikanaji wa huduma kwa wakulima wadogo, huku yakipunguza changamoto za kifedha zilizokuwa kikwazo kwa maendeleo yao.
Bw. Rugamba aliongeza: “Kupitia ushirikiano huu, tunaweza kupanua huduma hizi na kuwafikia maelfu ya wakulima nchini kote. Tunajibu moja kwa moja wito wa Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, alioutoa Desemba 2023, akiitaka sekta binafsi kushirikiana kwa karibu na wakulima wadogo ambao wengi wao hulima chini ya ekari 2.5, na wanahitaji msaada wa kubadilika kibiashara.”
Kwa upande wake, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege, alisema: “Makubaliano haya yanaashiria hatua muhimu katika kuimarisha maendeleo ya sekta ya ushirika na kilimo nchini. Kwa kushirikiana na Airtel Money, tunatoa fursa kwa wakulima wetu kustawi na kuendelea kuchangia kikamilifu katika uchumi wa taifa.”
Ushirikiano huu pia utawezesha ushiriki wa Airtel Money katika majukwaa mbalimbali ya kitaifa ya kilimo kama vile Maonesho ya Nane Nane, Siku ya Kimataifa ya Ushirika (ICUD), na matukio mengine muhimu yanayoandaliwa na TCDC, hivyo kusaidia kupanua zaidi wigo wa ujumuishwaji wa kifedha vijijini.
Kwa kuweka malipo ya wakulima kwenye mfumo wa kidijitali, na kutoa elimu na nyenzo za kifedha, ushirikiano huu kati ya Airtel Money na TCDC unatarajiwa kubadilisha maisha ya wakulima wa vijijini, kuongeza tija ya kilimo, na kuchochea mabadiliko ya kweli katika mustakabali wa sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa Airtel Money, Bw. Andrew Rugamba (wa pili kushoto), akibadilishana hati za makubaliano (MoU) na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk. Benson Ndiege, katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo kupitia huduma za mawasiliano na huduma fedha kidijitali. Ushirikiano huu unalenga kuwawezesha wakulima kupata huduma salama na za haraka za malipo, kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kupanua upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu, hususan katika maeneo ya vijijini. Wengine ni Mkurugenzi wa Sheria wa Airtel Tanzania, Bw. David Lema (kushoto), na Mwanasheria wa TCDC, Bw. Harry Mbogoro. Hafla hiyo ilifanyika mjini Dodoma jana.

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk. Benson Ndiege (kulia), akizungumza katika hafla ya utiaji saini hati za makubaliano kati ya tume hiyo na Kampuni ya Airtel Tanzania yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo kupitia huduma za mawasiliano na huduma fedha kidijitali. Ushirikiano huu unalenga kuwawezesha wakulima kupata huduma salama na za haraka za malipo, kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kupanua upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu, hususan katika maeneo ya vijijini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Airtel Money, Bw. Andrew Rugamba. Hafla hiyo ilifanyika mjini Dodoma jana.

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk. Benson Ndiege (aliyeketi kulia), Mkurugenzi wa Airtel Money, Bw. Andrew Rugamba (aliyeketi Katikati), wakipiga picha ya kumbukumbu katika hafla ya utiaji saini hati za makubaliano kati ya tume hiyo na Kampuni ya Airtel Tanzania yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo kupitia huduma za mawasiliano na huduma fedha kidijitali. Ushirikiano huu unalenga kuwawezesha wakulima kupata huduma salama na za haraka za malipo, kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kupanua upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu, hususan katika maeneo ya vijijini. Hafla hiyo ilifanyika mjini Dodoma jana.
No comments:
Post a Comment