BINTI FILAMU YAUNGA MKONO SERIKALI SEKTA YA AFYA - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Thursday, February 1, 2018

BINTI FILAMU YAUNGA MKONO SERIKALI SEKTA YA AFYA

Uongozi wa Taasisi ya Binti filamu Fondation umetoa Msaada wa Vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 30 katika hospitali ya Mwananyamala Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Meya  wa Kinondoni akizungumza na wadau na kutoka Taasisi ya Binti Filamu Fondution.

Akizungumza Jijini Dar es salaam leo Mstahiki Meya Manispaa hiyo Benjamin Sitta amesema,ameushukuru uongozi huo,kwa kutoa msaada huo katika hospitali hiyo na kusema kuwa kitendo hicho kimeonyesha ukomavu katika sekta ya filam kwa kutumika ipasavyo katika jamii na kuleta matokeo mazuri.
DSC_2829

Amesema  wasanii wanauwezo mkubwa wa ushawishi katika makundi tofauti katika jamii na kusema kuwa kama watatumika vizuri wataleta maendeleo makubwa .
DSC_2874
"Upo uwezekano kwa wasanii wa filamu nchini na wasanii wa aina zote wakatumika positively (vizuri) kwenye jamii na wakaleta impact (matokeo)kubwa" amesema Sitta
DSC_2795
Aidha Sitta amesema tukio hilo liwe chachu kwa wasanii wa aina nyingine ili wajue kuwa nguvu yao katika jamii ni kubwa na sio kufanya matukio kwenye mitandao ya kijamii.
DSC_2651
"matukio wanayo yafanya yanaleta athari kubwa kwa hawa vijana wadogo ambao tunawahangaikia wapate elimu bure, wasome  wanaendelea kukosa mwelekeo kwasababu wanaona Role Models wao mafanikio yao wanayapeleka kwenye mambo ya ajabu ajabu na kibaya zaidi sikuhizi kitu kidogo kwenye mitandao kinaenea kwa haraka zaidi  "Amesema Sitta
DSC_2676
Hata hivyo Siitta amewaahidi kuwapa ushirikiano katika nyanja tofauti kwa kuwakutanisha na wadau watakao watakaowahitaji hivyo amewataka kuleta mawazo yao yatakayofaa kwa manufaa ya jamii nzima.
DSC_2874
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dr. ISDORY KIWALE  ametoa shukrani zake za dhati  kwa uongozi wa Tasisi hiyo kwa msaada huo na kusema kuwa sio mara yao ya kwanza kufika hospitalini hapo na kutoa msaada hivyo wamekuwa na mchango mkubwa katika Hospitali hiyo.
DSC_2805
"Mwaka jana tulikuwa na shida ya Damu hivyo Wasanii hao walijitokeza na kuchangia Damu lakini na leo wamefika hapa na kutupatia vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 30 na sisi tunawaahidi vifaa hivi vitatumika kwa uangalifu mkubwa sana"Amesema Dr ISDORY
DSC_2835
Amesema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa na serikali bado wanahitaji watu ili wawasaidie katika nyanja tofauti za kuwapatia  vifaa tiba.
DSC_2696
Mlezi wa Taasisi hiyo Mama Asha Baraka akizungumza katika hafla hiyo

Kwa upande wake Mlezi wa Taasisi hiyo Mama Asha Baraka amesema  kuwa lengo lao kubwa ni kuisaidia jamii ,hasa akina mama na watoto ambapo pia ni harakati za kumuunga Mkono  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kwa  kuwapa vipaumbele wazee na akina mama wasio na uwezo.


MATUKIO KATIKA PICHA
IMG_5086

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages