Sunday, January 28, 2018
MSIKITI MKUBWA WA KISASA KUJENGWA ZINGIZIWA
Picha ya ramani ikionyesha namna msikiti wa Al-rahma utakavyo kuwa baada ya kukamilika.
Shek Nasr Tahdhanmy wakwanza kulia, akishudia utiaji saini wa kujenzi wa msikiti eneo la Chanika Zingiziwa yaliyofanyika Upanga jijini Dar es salaam.
Picha ya ramani ikionyesha namna msikiti wa Al-rahma utakavyo kuwa baada ya kukamilika.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya utiaji saini ujenzi wa msikiti wakionesha Picha ya
ramani ikionyesha namna msikiti wa Al-rahma utakavyo kuwa baada ya kukamilika.
Picha mbalimbali zikionyesha sehemu ambayo utajengwa Msikiti huo
Shek Nasr Tahdhanmy, akioneshwa eneo utakapo jengwa msiki zingiziwa Chanika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
Taasisi ya AL-NOOR CHARTABLE AGENCY, leo imesaini makubaliano ya Ujenzi wa Msikiti mkubwa utakao jengwa katika eneo la Zingiziwa Chanika jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo iliyo fanyika katika msikiti wa Mahmuor Upanga jijini Dar es Salaam, Shekh. Nasr Tahdhanmy, amesema, ujenzi huo utaanza kesho na utakamilika ndani ya miezi mitatu na utajulikana kwa jina la Masjid Al -rahma, utakuwa na uwezo wa kuswali watu 500 ndani na nje.
Amesema,wameamua kujenga msikiti huo katika eneo hilo kwa kuwa kuna Waislamu wengi na hawana Msikiti hivyo watuwengi watapata pahala pazuri pa kuabudu kuliko hivi sasa ambapo wanapatashida .
Msikiti huo utakuwa mkubwa , utakuwa na Maduka ,Clinic, sehemu ya kuoshea Maiti , nyumba ya mayatima Pamoja na nyumba ya Imamu.
‘’Nashukuru sehemu hii nikubwa Masha- allha na inawaislamu wengi kama tulivyo ambiwa, na msikiti kuja kuujenga huku mbali niliona siyo fikra nzuri lakini nilipo kuja kushauriana na wenzangu nikaona nifikra nzuri tumeuchukua msikiti kuwa fuata Waislam kuliko Waislamu kuufuata msikiti, alisema.
Naye Mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo Nadir Mahfoudh amesema kujenga msikiti kuwa fuata Waislamu nijambo zuri kuliko kuendelea tu kujenga misikiti maeneo ambayao yako karibu na barabara kuu, na sehemu hiyo ameona inafaa sana na kwamba malipo yatafanyika ili ujenzi huo uweze kuanza mara moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment