TEACHERS JUNCTION YAONGEZA JUHUDI YA UFAULU KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Wednesday, May 30, 2018

demo-image

TEACHERS JUNCTION YAONGEZA JUHUDI YA UFAULU KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI

IMG_3313
 Jumla ya  shule 45 kutoka katika mikoa 13 nchini zikiwemo za Serikali ambazo nazo zimefanya vizuri katika mtihani wa Darasa la Nne na la Sita.

Akiongea wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza na kuwapa zawadi baadhi ya watoto waliojitokeza kuhudhuliria katika hafra hiyo, Hafisa Miradi wa Taasisi ya Teachers Junctions Njama Salim amesema Mradi huu ulianzishwa Mwaka 2017 chini ya Usimamizi wa Taasisi hiyo ikiwa na lengo la kuimarisha upimaji wa wanafunzi kwa upande wa Shule za Msingi za watu binafsi pamoja na zile za serikali.

Amesema katika Mashindano ha shule ya Ubungo ya Tigohane imeibuka kidedea kwa kuchukua ushindi wa jumla kwa Mtihani wa darasa la Nne na kuongeza kuwa Watoto wote walioshiriki Mtihani huo walikua katika Mchuano mkali.

Amesema Lengo Kubwa la Mtihani huo ni kuisaidia Serikali katika kuwapima wanafunzi na kwamba kwa mara ya kwanza wameweza kupata ushiriki mzuri kutoka katika shule za Serikali zinazotumia Mtaala wa kingereza.

Upande wake Msemaji kutoka shule ya wavulana ya Sullivan Provost kwa niaba ya Mkuu wa shule Felix Kavishe, amesema kuwa wataendelea kuunga mkono mashindano hayo kwani yanaleta chachu ya ufaulu. 

Mradi wa INTERSCHOOL EXAMS AND CONSULTANCY ni Mradi wa miaka Mitatu na unalenga katika kutoa ushauri na kuhamasisha wanafunzi kwa kuwapatia Zawadi mbalimbali hasa we
ale wenye wastani Mkubwa.

IMG_3452
Baadhi ya wanafunzi waliohudhulia hafla hiyo na baadhi yao wameibuka washindi katika mitihani yao ambayo, katika mashindano hayo Shule 45 zimeshiriki mashindano hayo.
IMG_3301
Mwanafuzi wa Darasa la nne katika Shule ya Msingi ya Junior iliyoko Mzumbe Morogoro Jackline Bahasha, akivalisha Medali ya ufauru wa jumla na Meneja wa Mauzo na Masoko wa New Habari 2006, Mrs Rehema Ahmed.
IMG_3294
Mwanafunzi wa Darasa la nne katika Shule ya Msingi ya Diamond iliyoko  Dar es Salaam Abdusalaam Selemani, akivalisha Medali ya ufauru wa jumla na Meneja wa Mauzo na Masoko wa New Habari 2006, Mrs Rehema Ahmed.
IMG_3356
Mwanafunzi wa Darasa la nne katika Shule ya Msingi ya Tigohane iliyoko Wilaya ia Ilala Dar es Salaam  Brian Richard, akipokea Ngao ya ushindi kwa kuongoza kwa masomo yote katika shule zilizoshindanishwa na Meneja wa Mauzo na Masoko wa New Habari 2006, Mrs Rehema Ahmed.
IMG_3287
Mwanafunzi wa Darasa la sita katika Shule ya Msingi ya Dominic Savio ya Iringa, Gloria Castro, akipokea Ngao ya ushindi kwa kuongoza kwa masomo yote katika shule zilizoshindanishwa katika masomo ya darasa la sita na Meneja wa Mauzo na Masoko wa New Habari 2006, Mrs Rehema Ahmed. mashindano hayo yalioanzishwa na Mradi wa  Teachers Junction.
IMG_3240
Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari ya wavulana Sullivan Provost, Felix Kavishe akizungumza na walimu wazazi pamoja na wanafunzi kwaniaba ya Mkuu wa shule hiyo Mr Alex Nichoraus wakati wa sherehe za kutoa tuzo kwa wanafunzi wa Darasa la sita na lanne waliofanya vizuri ikiwa shule ya Sullivan ilikuwa wadhamini wakuu ambapo waliandaa Ngao kwaajili ya darasa la sita katika mashindano hayo Shule 45 walishiriki  hayo yalioanzishwa na Mradi wa  Teachers Junction.

IMG_3415
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wavulana Sullivan Provost, akitoa neno kwa wanafunzi waliohudhulia mashindano hayo nakuwasihi kama wakitaka kuendelea vizuri na ufaulu wao basi wachague shule ya Sullivan kwaajili ya kupata elimu bora mashindano hayo yalioanzishwa na Mradi wa  Teachers Junction.
IMG_3212
Afisa Mradi wa Teachers Juction Njama Salum akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo shule 45 walishiriki mashindano hayo.


IMG_3346
Mkuu wa Shule ya Msingi Tigohane iliyoko Wilaya ia Ilala Dar es Salaam   Meleck Macha alielala chini, akibubujikwa na machozi baada yakutangazwa kuwa Mwanafunzi wa  shuleyake Brian Msangi,  ameibuka kidedea nakujinyakulia Ngao ya ufaulu katika mitihani yote kwa darasa la nne, Shule 45 zimeshiriki mashindano hayo.
IMG_3391
Mkuu wa Shule ya Msingi ya Dominic Savio Sister Beatrice Kapinga, Iringa, akitoa neno la shurani kwa uongozi wa Shule ya Sekondari ya wavulana Sullivan Provost, kwakuona umuhimu wa mashindano hayo na kuandaa ngao hiyo kwa wanafunzi wa darasa la sita ambayo shule ya Dominic Savio ndio imenyakua ngao hiyo kupitia mwananzi wake Gloria Castro ameibuka kidedea nakujinyakulia Ngao ya ufaulu katika mitihani yote kwa darasa la sita, ambapo Shule 45 kutoka mikoa 13 nchin


MATUKIO KATIKA PICHA
IMG_3451


IMG_3213


IMG_3453


IMG_3452
IMG_3205
Wanafunzi wa Shule ya Wavulana na Sullivan wakiwa katika hafla hiyo.
IMG_3213


IMG_3215


IMG_3216


IMG_3245


IMG_3247


IMG_3308


IMG_3310


IMG_3311


IMG_3312


IMG_3313




IMG_3316


IMG_3337




IMG_3352


IMG_3370


IMG_3373

IMG_3400
IMG_3404


IMG_3494

No comments:

Post a Comment

 Jumla ya  shule 45 kutoka katika mikoa 13 nchini zikiwemo za Serikali ambazo nazo zimefanya vizuri katika mtihani wa Darasa la Nne na la Sita. Akiongea wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza na kuwapa zawadi baadhi ya watoto waliojitokeza kuh...

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *