Majaliwa kuwa mgeni rasmi mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Kuruan - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Friday, June 1, 2018

Majaliwa kuwa mgeni rasmi mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Kuruan

1%2B%25281%2529

ddddddddddd



WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika fainali za  Mashindano  makubwa  ya 26 ya Kusoma na Kuhifadhi Kuruan Tukufu Duania.

Mbali na majaliwa, viongozi wengine watakaohudhuria fainali hizo zitakazofanyika katika ukumbi wa Diamond  DiamondJubilee, kesho,  jijini Dar es salaam ni  marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Dk. Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Mstaafu Dk. Mohammed Gharib Bilal

Akizungumza jijini na waandishi wa habari,, Mratibu wa mashindano hayo,  Sheikh Mohammed  Nasoro,  kutoka Taasisi ya Kuhifadhisha Kuruan TukufuTanzania ambao ndiyo wandaaji wa mashindano hayo,   amesema jumla ya nchi18 zitashiriki.

 Amezitaja baadhi ya nchi hizo kuwa ni Tanzania, Saud Arabia, Mali, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Malawi, Congo DRC,  Russia, Sylia, Yemen, Malaysia, Bangladesh, Uingereza, na Burundi.

“Washiriki wote wamewasili nchini  ambapo juzi na jana tuliwafanyia mashindano ya mwisho ya kupata wale bora ambao wataingia katika fainali kesho,”alisema Sheikh  Nasoro.
Alisema, majaji watatoka nchi za Uingereza, Yemen, Saud Arabia  na Sudan na tayari wamewasili nchini.

“Zawadi tutatangaza baadaye ingawa pia fainali hizo zitakwenda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima  kwa watu mbalimbali,”alibainisha.

Katibu wa Taasisi ya Kuhifadhisha Kuruan Tukufu Tanzania, Mohammed Ally Hassan, amewaomba watanzania kushiriki kwa wingi kwani jambo hilo ni la kheri hasa katika kipindi hiki cha Ramadhan.

Akizungumza kwa niaba ya jopo la majaji wa fainali hizo, Jaji Dk. Abbas Hamza kutoka nchini Sudan , amesema wanaamini haki itatendeka na kuwataka watanzania kuhudhuria kwa wingi.

No comments:

Post a Comment

Absa Dar City Marathon 2024 zatimua vumbi jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga (kushoto), akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za nu...

Pages