WAITARA AFANYA UKAGUZI WA UJENZI WA MIUNDO MBINU UKONGA - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Tuesday, June 12, 2018

WAITARA AFANYA UKAGUZI WA UJENZI WA MIUNDO MBINU UKONGA

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa Beach Pemba kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam jana katika ziara yake ya ukaguzi wa miundo mbinu inayotengenezwa  pamoja na kusiliza kero za wakazi wa kata hiyo.Moja ya Miundo mbinu inayotengenezwa Beach Pemba ni ujenzi wa mifereji ya chini kwa chini ambayo inatoa maji ya mvua yanayotuama katika eneo hilo na kumwaga moja kwa moja katika bonde la mto Mzinga.Wanne kulia ni Diwani wa kata hiyo Job Isaack.
Diwani Viti maalumu Manispaa ya Ilala, Sara Katanga akizungumza jambo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya kero ya kutuama kwa maji ya mvua katika eneo la Beach Pemba kata ya Mzinga ambayo imefanyiwa utatuzi kwa kutengenezwa mifereji ya chini kwa chini  itakayo yaongoza maji hayo moja kwa moja katika Bonge la Mto Mzinga.
Mkazi wa Beach Pemba, Alhaji Hassani Magogwa akitoa shukrani za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (hayupo pichani) baada ya kutatua kero ya maji ya mvua yanayotuama katika eneo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (ailyevaa shati la kaki) akiongozana na wakazi wa kata ya mzingo baada ya kumaliza kukagua mradi wa Beach Pemba.
Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa kituo Kikubwa cha Polisi kata ya Mzinga, Godfrey Mujungu (kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (watatu kushoto) baada ya kuwasili katika kata hiyo kwa aijli ya ukaguzi wa ujenzi wa Kituo hicho kinachotengezwa kwa nguvu ya wananchi kutoka katika mitaa mitatu ambayo ni Mwanagati, Mzinga na Magole. Wapili kulia ni Diwani wa kata hiyo, Job Isaack na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mzinga, Mussa Mtani.

Msimamizi wa ujenzi wa kituo Kikubwa cha Polisi upande wa wakazi wa kata ya Mzinga, Nasir Suleiman (kushoto) akimuonesha Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kipo katika msingi.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Kituo cha Kikubwa cha Polisi cha kata ya Mzinga.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akifanya ukaguzi wa ujenzi wa Barabara inayounganisha Kitunda, Kivule na Msongola.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akizungumza na msimamizi wa ujenzi wa Barabara inayounganisha Kitunda,Kivule na Msongola baada ya kuwasili maeneo ya Matembele kata ya Kivule katika ziara yake ya ukaguzi wa miundo mbinu inayotengenezwa jimboni jijini Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (wapili kulia) akiongozana na Diwani wa kata ya Kivule, Wilson Molel (watatu kulia) pamoja na viongozi wengine wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuelekea katika ujenzi wa Daraja la Mto Mzinga katika hafla yake ya ukaguzi wa miundo mbinu inayotengenezwa jimboni.

 Daraja la Mto Mzinga likimaliziwa kuwekwa kifusi.

 Mkazi wa Kata ya Kivule akitoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia) kwa kutatua kero ya Daraja la Mto Mzinga ambalo lilikuwa ni kikwazo kikubwa cha shughuli za kiuchumi na kijamii kuwa ngumu kwa sababu gari zilikuwa hazivuki kutokana na kuvunjika kwa daraja hilo.Huu ni mwendelezo wa Mbunge kutimiza ahadi ambazo aliziahidi kwa wakazi wa jimbo la Ukonga.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia) akiongozana na Diwani wa kata ya Kivule, Wilson Molel katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Daraja la Mto Mzinga.
Diwani wa kata ya Kivule, Wilson Molel (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika ziara ya Mbunge wa Jimbo la Ukonga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi wa Barabara Mabibo Construction Company Limited, Charles Werongo akizungumza katika ziara ya Mbunge wa Jimbo la Ukonga.Mkurugenzi alisema baada ya wiki tatu Daraja litakuwa tayari kwa aijli ya matumizi ya wananchi.
Mkazi wa kata ya Kivule pia Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa kata hiyo, Bihimba Mpaya akitoa neno la Shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara pamoja na Diwani wa kata hiyo, Wilson Molel kutoka na juhudi walizozifanya juu ya kupambana na kero ya  Daraja la Mto Mzinga ambayo ilikuwa ni kikwazo kikubwa kwa wakazi wa kata hiyo pamoja na wafanyakazi wa Taasisi za Kijamii kama Walimu,Madaktari ilikuwa ni ngumu sana kufika maeneo ya kazi mapema kutokana gari kuishia kati kutokana na kukatika kwa Daraja hIvyo kwa Juhudi za Mbunge na Diwani wake kero imetatulika kwa muda mfupi.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages