RC MAKONDA APIGA MARUFUKU KAMPUNI YA UJENZI YA NYANZA KUPEWA MRADI DAR ES SALAAM, NI BAADA YA KAMPUNI HIYO KUZIDISHA "UBABAISHAJI" - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Saturday, November 2, 2019

RC MAKONDA APIGA MARUFUKU KAMPUNI YA UJENZI YA NYANZA KUPEWA MRADI DAR ES SALAAM, NI BAADA YA KAMPUNI HIYO KUZIDISHA "UBABAISHAJI"


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda Novemba 02 amewataka TANROAD kuhakikisha Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza haipatiwi mradi wowote wa ujenzi ndani ya mkoa huo baada ya kampuni hiyo kuendelea kusuasua kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Barabara ya Kivule licha ya Kupewa fedha za ujenzi.

RC Makonda ametoa onyo hilo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambapo akiwa kwenye barabara ya Kivule yenye urefu wa Km 3.2 ameshuhudia Mkandarasi huyo akiwa na uhaba wa Vifaa licha ya kudanganya kwenye mikataba kuwa anavyo vifaa vya kutosha ili apatiwe tenda jambo lililopelekea mradi kuchukuwa muda mrefu bila kukamilika.

Aidha RC Makonda amesema mradi huo ndio utakuwa wa mwisho kwenye mkoa huo huku akizionya bodi za manunuzi zinazotoa tenda Kwa kuendekeza Rushwa na kujuana jambo linalowafanya kushindwa kumuonya mkandarasi kwakuwa tayari wamefungwa midomo Kwa rushwa.

Katika ziara hiyo RC Makonda ametembelea ujenzi wa Machinjio mpya ya Vingunguti ambapo ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo ambao kwa sasa upo kwenye hatua ya kufunika gorofa ya kwanza huku akieleza kuwa anaamini ujenzi utakabidhiwa Mwezi Disemba.


Katika hatua nyingine RC Makonda ametembelea ujenzi wa Mto Sinza na Mto Ng'ombe wenye urefu wa Km 7.5 ambao baada ya kuwakamata wakandarasi hatimae ujenzi sasa umeanza huku akimtaka mkandarasi wa kampuni hiyo kumaliza mradi kwa wakati.

Pamoja na hayo RC Makonda amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya NAMIS Corporate LTD inayojenga Soko la Tandale kukamilisha ujenzi huo haraka ili wafanyabiashara wauze bidhaa katika sehemu nzuri.

Itakumbukwa kuwa October 24 RC Makonda aliagiza kukamatwa Kwa wakandarasi wa kampuni ya CHICO na Nyanza baada ya kampuni hizo kusuasua kwenye miradi Kwa muda mrefu na hatimae sasa wakandarasi wameingia kazini.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Biashara DCB kuendelea kuboresha Maisha ya Watanzania

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bias...

Pages