RC MAKONDA AFANIKISHA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO 500 WENYE TATIZO LA MOYO - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Thursday, October 31, 2019

RC MAKONDA AFANIKISHA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO 500 WENYE TATIZO LA MOYO


Ubalozi wa Nchi za Falme za Kiarabu UAE umeendelea kuunga mkono kampeni ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto kutoka familia duni Iliyoanzishwa na  Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Makonda ambapo leo October 31 wamemkabidhi hundi ya Shilingi Milioni 27 kwaajili ya Bima za Afya kwa Watoto 500 wenye Tatizo la Moyo.

RC Makonda amesema kiasi hicho cha fedha kitawezesha Watoto 500 wakiwemo yatima na Wanaotokea familia duni Waliolazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kupata Bima za Afya zitakazowawezesha kupata Matibabu Bure kwa kipindi cha Mwaka Mzima.

Aidha RC Makonda amesema uamuzi wa kuwatafutia Bima za Afya umekuja baada ya kubaini Watoto wengi wanaofanyiwa upasuaji wanahitajika kwenda Clinic kwaajili ya kufuatilia maendeleo ya Afya na Dawa lakini kutokana ugumu wa maisha wanashindwa kumudu gharama jambo linalowafanya Wazazi au Walezi wao kuuza Mali walizochuma kwa muda mrefu ili wapate fedha na mwisho wa siku familia inazidi kuwa maskini.


Pamoja na hayo RC Makonda amemshukuru Balozi kwa kuendelea kumuunga mkono katika mambo mbalimbali ikiwemo kusomesha watoto 100 wa kike kidato cha tano na sita, Kumpatia madaktari bingwa wa Moyo Waliofanya upasuaji kwa watoto 60, Kumsaidia futari kwaajili ya Maimamu wa Misikiti 800 huku akitoa wito kwa Wananchi kuwa na moyo wa upendo wa kusaidia wenye uhitaji.


Kwa upande wake Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu Bw. Khalifa Abdulrahman Almarzooqi amesema kuwa Ubalozi huo unafurahishwa na kazi nzuri ya RC Makonda katika kusaidia Wananchi wenye uhitaji ndio maana wameamua kushirikiana nae kwa kila jambo kwakuwa kila msaada anaoupokea unawafikia walengwa.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Biashara DCB kuendelea kuboresha Maisha ya Watanzania

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bias...

Pages