Thursday, October 31, 2019
NBC kuendelea kuwapiga jeki wanawake wajasiriamali nchini
Waziri Mkuu Mstaafu,
Mizengo Pinda akikabidhi cheti cha shukrani kwa Kaimu Mkurugenzi wa Wateja
Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kushoto), kwa
kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kongamano la wanawake
lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa
kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta
Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar
es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1, Jumbe Menye.
Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya (kulia), akizungumza na Meneja
Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Chiku Chambuso (kushoto),
pamoja na mwenzake, Lena Mwakisale katika banda la benki hiyo wakati wa kongamano
la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa
kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta
Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar
es Salaam jana.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Meneja
Mahusiano Wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Lena Mwakisale pamoja
mwenzake Isdory Maumba (kushoto), alipokutana nao wakati wa kongamano la
wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa
kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta
Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo ililidhamini na kufanyika jijini Dar
es Salaam jana.
Waziri Mkuu Mstaafu,
Mizengo Pinda akihutubia wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la
‘Madirisha’ lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya
Sekta Binafsi (TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS)
ambalo Benki ya NBC ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi wa
Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Benjamin Nkaka (kulia),
akishikana mikono na Kaimu Mwenyekiti Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF),
Angelina Ngalula wakati wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’
lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi
na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo
ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa
Bodi ya GS1, Jumbe Menye.
Baadhi ya wanawake
waliohudhuria wa kongamano la wanawake lililopewa jina la ‘Madirisha’
lililoandaliwa na Kampuni ya GS1 kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi
(TPSF), na Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS) ambalo benki hiyo
ililidhamini na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
NA Mwandishi Wetu,
Dar
BENKI
ya Taifa ya Biashara (NBC) imewataka wafanyabiashara na wajasiriamali wanawake
nchini kuondoa hofu ya kutembelea na kuzungumza na wataalamu wa masuala ya
fedha na biashara katika matawi ya benki hiyo ili kufahamu huduma zao na jinsi
wanavyoweza kupata huduma za kifedha zitakazoweza kuinua biashara na maisha yao.
Akizungumza
wakati wa Kongamano la Kwanza la Wafanyabiashara Wanawake wakubwa na wa kati
jijini Dar es Salaam jana ambao benki hiyo ililidhamini, Kaimu Mkurugenzi wa
Wateja Binafsi wa NBC, Benjamin Nkaka, alisema ni vyema kwa wafanyabishara hao
wanawake kuzoea kufanya kazi na benki kwani ni njia rahisi na pekee itakayoweza
kustawisha biashara zao.
“Kuna
hofu imejengeka kwa wengi kuja benki. Hofu hiyo iondoke. Njooni benki muweze
kufahamu ni nini tunakitoa katika kusapoti wajasiriamali hasa wanawake,”
alisema Nkaka.
Alisema
miongoni mwa majukumu ya benki hiyo ni kusaidia katika kukuza uchumi hasa wa
wanawake wajasiriamali, na kuongeza:
“Kwa
zaidi ya miaka 50 ya huduma za benki hii nchini, tunafahamu kuwa miongoni mwa
changamoto zinazowakabili wajasiriamali
wanawake ni elimu ya mikopo. Sisi tunatoa elimu hiyo pamoja na ushauri kwa
wateja wetu wafanyabiashara kadri biashara yao inavyoendelea na kuwaunganisha
na mnyororo wa thamani.
“NBC
pia huwakutanisha wateja na wadau mbalimbali kama vile Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA), Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara (BRELA) na taasisi nyingine.
Katika harakati zetu za kuwasapoti wanawake, tumeanzisha Vikundi Akaunti ambazo
hazina makato yoyote, huku pia tukishirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi ya
Kilimo (PASS) kutoa mikopo yenye garantii ya hadi asilimia 80 kuwawezesha
wanawake kuingia kwenye kilimo kwa nguvu.”
Mkutano
huo ulihudhuriwa na takriban wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara 1,000
kutoka mikoa yote ya Tanzania huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu mstaafu,
Mizengo Pinda.
Wanawake
hao walikutanishwa kupitia mwavuli unaofahamika kama ‘Madirisha’ huku wadau mbalimbali
wa maendeleo wakipata nafasi ya kuwaonyesha wanawake hao fursa mbalimbali
zilizopo nchini katika kuboresha uchumi wao kama vikundi.
Kampuni
ya GS1 iliandaa kongamano hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi
nchini (TPSF) pamoja na taasisi ya PASS.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Biashara DCB kuendelea kuboresha Maisha ya Watanzania
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bias...
No comments:
Post a Comment