MKUTANO WA MAWAZIRI WA KAMATI YA SADC YA ASASI YA USHIRIKIANO WA SIASA, ULINZI NA USALAMA WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Thursday, June 25, 2020

MKUTANO WA MAWAZIRI WA KAMATI YA SADC YA ASASI YA USHIRIKIANO WA SIASA, ULINZI NA USALAMA WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na baadhi ya Maafisa waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano huo kwa njia ya Video Conference, jijini Dar es Salaam.
Washiriki wakifuatilia mkutano kwa njia ya Video Conference jijini Dar es Salaam

Mkutano wa Mawaziri wa Kamati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa ngazi ya Makatibu Wakuu/ Maafisa Waandamizi umefanyika tarehe 25 Juni,2020, Jijini Dar es Salaam kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing).

Mhimili wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC unaongozwa na mfumo wa Utatu (Troika) ambapo kwa sasa Mwenyekiti ni Zimbabwe, mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu unaofanyika leo ni maandalizi ya mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 26 Juni 2020 chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Sibusiso Busi Moyo na utakutanisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mambo ya Ndani, Ulinzi na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka nchi wanachama wa SADC.

Pamoja na mambo mengine mkutano umepokea na kujadili agenda zinazohusu masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Ukanda wa SADC.Mkutano wa leo umehudhuriwa na nchi wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, DRC,  Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Zambia, Zimbabwe na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ni moja ya mihimili ya SADC inayosimamia masuala ya Usirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Kanda. Mhimili huu unatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Mkataba wa uanzishwaji wa SADC wa mwaka 1992 na Itifaki ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ya mwaka 2001.

No comments:

Post a Comment

SIMTANK TANZANIA YATOA ZAWADI KWA MAWAKALA WAKE WAKISHEREHEKEA MIAKA 35 TANGU KUANZISHA

    Mwanzilishi wa Kampuni ya Silafrika Tanzania inayozalisha bidhaa za Simtank, Gulab Shah (wapili kushoto), akikabidhi cheti na zawadi ya ...

Pages