RAIS MWINYI AJUMUIKA WANAFAMILIA NA WANANCHI KUUPOKEA MWILI WA MAREHEMU ISSA KASSIM ISSA (BAHARIA) BANDARINI ZANZIBAR - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Saturday, December 18, 2021

RAIS MWINYI AJUMUIKA WANAFAMILIA NA WANANCHI KUUPOKEA MWILI WA MAREHEMU ISSA KASSIM ISSA (BAHARIA) BANDARINI ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi na Wanafamilia katika kuupokea Mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) aliyefariki leo 18-12-2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akielekea katika Bandari ya boti za abiria wanaotokea Dar es Salaam kwa ajili ya kuupokea Mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa, aliyefiri leo 18-12-2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam, akipatiwa matibabu.(kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar. Mhe.Rahma Kassim Ali na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe Simai Mohammed Said. (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwafariji na kutowa mkono wa pole kwa Watoto wa Marehemu Issa Kassim Issa, alipofika Bandari Malindi kwa ajili ya kuupokea mwili wa Marehemi Issa Kassim Issa (Baharia) aliyefariki leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam akipatiwa matibabu. (Picha na Ikulu)
WANAFAMILIA na Wananchi wakipokea mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) katika bandari ya Malindi Zanzibar baada ya kuwasili na Boti ya Azam Marine, ukitokea Dar es Salaam. (Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages