USHINDI WA BIKO WATUA KWA HASHIMU WA LUGOBA - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, December 1, 2021

USHINDI WA BIKO WATUA KWA HASHIMU WA LUGOBA

 
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akifurahia jambo na Hashimu Shabani wa Lugoba mkoani Pwani aliyeshinda fedha za bahati nasibu ya Biko sh milioni 10. Makabidhiano hayo yamefanyika Kibaha, mkoani Pwani. Picha na Mpigapicha wetu.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akifurahia jambo na Hashimu Shabani wa Lugoba mkoani Pwani aliyeshinda fedha za bahati nasibu ya Biko sh milioni 10. Makabidhiano hayo yamefanyika Kibaha, mkoani Pwani.
Balozi wa Biko Kajala Masanja akiwa na mshindi wa sh milioni 10 Hashimu Shabani wa Lugoba mkoani Pwani kushoto kwake. Wengine ni marafiki wa Hashimu waliokuwa wanampongeza kwa ushindi wake. Picha ma Mpigapicha wetu.

Mwandishi Wetu, Chalinze | Mkazi wa Lugoba, wilayani Chalinze mkoani Pwani, Hashimu Shabani, amekabidhiwa fedha zake sh milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa ya bahati nasibu ya Biko inayoongoza kutoa washindi wengi sehemu mbalimbali za Tanzania wanaocheza kwa kuanzia sh 1000 na kuendelea.

Makabidhiano hayo yamefanyika mkoani Pwani na kuongozwa na balozi wa Biko Kajala Masanja na kusema biko ni mchezo unaosambaza mamilioni ya fedha kwa Watanzania wanaocheza live kwa njia ya mtandao www.biko.co.tz pamoja na wanaotumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 au neno biko.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Shabani alisema kuwa fedha zake hizo ataziingiza kwenye mradi wake wa kumiliki bodaboda ili ziweze kumsaidia katika maisha yake, akiamini kuwa bahati kama hiyo inaweza isijirudie tena.

Namshukuru Mungu kwa kunipatia fursa hii ya kushinda zawadi nono ya Sh Milioni 10 kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko, hivyo wakati huu ambao maisha ni magumu mtaani, nimeamua kununua bodaboda nikiamini zinaweza kuniokoa".

Siwezi kufanya makossa, maana Mungu mwenyewe ndiye anayejua kwanini ameamua kunipa ushindi wa Biko, ingawa nilicheza nikiwa na Imani kubwa kama kuna siku ningeweza kuibuka mshindi kama wanavyoshinda wengine,” Alisema.

Naye Balozi wa Biko, Kajala Masanja amesema kuwa wakati huu wa kuelekea kufunga mwaka 2021, Watanzania wote wanaocheza biko wana nafasii kubwa ya kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja na ofa kibao zikiwamo za mamilioni kila Jumapili.

Biko ni mchezo wa kubahatisha unaoongoza kutoa fedha nyingi kwa Watanzania, ambapo zwadi za papo kwa hapo zinatoka kila sekunde moja kuanzia sh 2500 hadi milioni 5 papo hapo bila kusahau kutoa zawadi ya hadi sh milioni 40 kila Jumapili ambapo mbali na kucheza kwa namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu 2456, pia watu wanaweza kucheza live kwa kuingia www.biko.co.tz.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages