FURSA MPYA ZA BIASHARA DRC: CRDB YAWA DARJA LA KUUNGANISHA WAFANYABIASHARA NA MASOKO - Business Insights

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +715765454 email: mgongo@gmail.com

Breaking

Tuesday, November 3, 2026

FURSA MPYA ZA BIASHARA DRC: CRDB YAWA DARJA LA KUUNGANISHA WAFANYABIASHARA NA MASOKO

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Nsekela, wameongoza ujumbe wa Benki ya CRDB katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Judith Suminwa Tuluka, yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo ni sehemu ya juhudi za kimkakati za Benki ya CRDB katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda, kuunganisha masoko na kufungua fursa mpya za biashara, uwekezaji na maendeleo kati ya Tanzania na DRC, na kwa upana zaidi, katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Mhe. Judith Suminwa Tuluka ameeleza utayari wa Serikali ya DRC kushirikiana na Benki ya CRDB katika maeneo mbalimbali ya kimkakati, akitambua nafasi ya sekta ya fedha katika kuharakisha maendeleo, kurahisisha biashara na kuchochea uwekezaji wenye tija kwa wananchi wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Uongozi wa Benki ya CRDB umesisitiza dhamira ya Benki kuwa mshirika wa kimkakati katika utekelezaji wa ajenda za maendeleo ya kikanda, ikiwemo kutumia fursa zinazotokana na Ushoroba wa Kati na Ushoroba wa Lobito kuimarisha biashara, uwekezaji na miunganiko ya kiuchumi. Juhudi hizi pia zitalenga kupanua wigo wa uwezeshaji kwa vijana, wanawake na biashara ndogo na za kati (SMEs).

Sambamba na hilo, Benki imethibitisha dhamira yake ya kuendelea kuwekeza nchini DRC na kupanua wigo wa huduma zake nje ya Lubumbashi na Kinshasa, hatua itakayoiwezesha kuwafikia wateja wengi zaidi na kushiriki kikamilifu katika fursa zinazochochewa na ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

Kupitia uwepo wake Tanzania, Burundi na DRC, Benki ya CRDB inazidi kujijenga kama taasisi ya kifedha yenye mtazamo na ushawishi wa kikanda, inayokwenda zaidi ya kutoa huduma za kibenki na kuchukua nafasi ya kuunganisha mitaji, biashara, wawekezaji na fursa za maendeleo katika Afrika Mashariki na Kati.

Kwa CRDB, mipaka si kikwazo cha fursa, bali ni daraja la kuunganisha uchumi, masoko na mustakabali wa maendeleo ya kikanda.

No comments:

Post a Comment

ARE YOUR MONEY AND FINANCES WORKING FOR YOU, OR ARE YOU WORKING FOR MONEY?

Understanding the Secrets of Effective Financial Management, Savings and Business Growth In everyday life, many people work hard to earn mon...

Pages