Thursday, July 27, 2017
NBC yazindua Klabu ya Biashara 'B-Club' mjini Kahama
Meneja Mahusiano wa Benki
ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa
Klabu ya Biashara ya benki hiyo mjini Kahama, Shinyanga jana. Klabu hiyo iliyopewa jina la 'B-Club'
imeanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Katikati
ni mmoja wa wateja, Salum Selemani na Joshua John (kulia), Ofisa Masoko wa
Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) kutoka ofisi ya
Mwanza.
Meneja Mahusiano wa Benki
ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa
mjini Kahama, katika semina iliyoandaliwa kabla ya uzinduzi rasmi
wa Klabu ya Biashara ya NBC hiyo iliyoanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja
wafanyabiashara wadogo na wa kati. Hafla ya uzinduzi ilifanyika mjiini Kahama,
Shinyanga jana.
Meneja wa Kanda wa NBC,
Daudi Mfalla (kulia), akizungumza wakati akizungumza katika hafla ya
uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC iliyoanzishwa kusaidia
mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Kushoto ni Mkuu wa
Kitengo cha Wafanyabiashara wadogo na wakati wa NBC, Evance Luhimbo.
Baadhi ya wateja wa NBC mjini Kahama waliohudhuria
uzinduzi wa B-Club ya benki hiyo, wakijipiga picha ‘selfie’ pamoja na bango lenye
picha inayoonyesha kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni baadhi ya shamrashara
zilizopamba uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa NBC tawi la
Kahama wakipozi kwa katika hafla hiyo.
Wasanii wakionyesha umahiri wao kucheza ngoma ya kadete
ya kabila la wasukuma katika hafla ya uzinduzi wa B-Club mjini Kahama,
Shinyanga jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment