Wednesday, August 2, 2017
ATE yaanza kundi la pili la Programu ya Mwanamke wa Wakati Ujao (Female Future)
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc, Sabasaba Moshingi
(katikati) akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered,
Sanjay Rughani wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya miezi tisa ya program ya
Mwanamke wa Wakati Ujao ya kundi la pili yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri
Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri
Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo yana lengo la kuwaandaa
wafanyakazi wanawake kushika nafasi za juu za uongozi katika makampuni na bodi
za wakurugenzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Bi. Jayne Nyimbo (wa pili kushoto),
Mkuu wa Idara ya Sheria ya ATE, Suzan Ndomba (kushoto) ma Mkurugenzi Mtendaji
wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka (katikati), wakifurahi na Mkuu wa Kitengo cha
mafunzo na maendeleo wa Acacia Mining, Janeth Lekashingo katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Bi. Jayne Nyimbo (kushoto),
akisalimiana na Mkurugenzu wa Kampuni ya Statoil Tz, Gunnar Mentzsen huku Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akiangalia wakati
wa uzinduzi wa mafunzo ya program ya Mwanamke wa Wakati Ujao
yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana
na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Taasisi ya Uongozi ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI), Prof. Apollonia
Kerenge (kulia), akizungumza na washiriki wa kundi la pili wa mafunzo ya miezi
tisa ya program ya Mwanamke wa Wakati Ujao yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri
Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shireikisho la Vyama vya Waajiri
Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo yana lengo la kuwaandaa
wafanyakazi wanawake kushika nafasi za juu za uongozi katika makampuni na
bodi za wakurugenzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate, Frank Mugeta
(kulia), akizungumza na washiriki wa mafunzo ya miezi tisa ya
program ya Mwanamke wa Wakati Ujao yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania
(ATE) kwa kushirikiana na Shireikisho la Vyama vya Waajiri Nchini
Norway (NHO) jijini Dar es Salaam juzi. Mafunzo yana lengo la kuwaandaa
wafanyakazi wanawake kushika nafasi za juu za uongozi katika
makampuni na bodi za wakurugenzi.
Mratibu wa Program ya Mwanamke wa Wakati Ujao ya Chama cha
Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Lilian Machera akizungumza na washiriki hao kuhusu
utaratibu wa mafunzo hayo yenye malengo ya kuwaandaa wafanyakazi wanawake
kushika nafasi za juu za uongozi katika makampuni na bodi za
wakurugenzi.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya program ya Wanawake wa Wakati
Ujao, Bi. Anna Nyimbo akijitambulisha kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo
yatakayochukua kipindi cha miezi tisa.
Washiriki wa kundi la pili la mafunzo ya program ya Mwanamke wa
Wakati Ujao wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya viongozi wa ATE
pamoja na wakurugenzi wa makampuni 16 yanayofadhili mafunzo hayo. Makampuni
hayo ni; Acacia Mining, Alistair Equipment Services (T) Ltd, AngloGold
Ashanti, Geita Gold Mine, Cartrack Tanzania Limited, EFC Microfinance Bank,
Ubalozi wa Denmark, Global Health Program-Tanzania, HJFMRI, Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC), Benki ya NMB Plc, Mfuko wa PPF , Songas Limited,
Benki ya Standard Chartered, Statoil Tanzania AS, Benki ya TIB Corporate, Benki
ya TPB Bank Plc na Under The Same Sun.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment