Saturday, August 19, 2017
TIB Corporate Bank katika jukwaa la biashara Tanga
Benki ya
TIB Corporate imeweza kushiriki jukwaa la biashara lililofanyika kwenye ukumbi
wa Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga ambapo kutoa fursa za namna ya benki
hiyo inavyoendesha shughuli zake hapa nchini.
Wakielezea
fursa hizo mbalimbali katika Mkoa wa Tanga, benki inajiweka sawa ili
kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia wana Tanga.
“Tunambua
kuwa maendeleo yoyote yale ya kibiashara na viwanda yanahitaji uwezeshwaji wa
kifedha (bank facilities). TIB Corporate Bank inatoa Huduma
mbalimbali kutokana na mahitaji ya Mteja.hii ni pamoja na akaunti mbalimbali za
kwa makampuni na Watu binafsi, mikopo ya aina mbalimbali ya muda mfupi na
muda wa kati, dhamana za kibenki ( bank guarantee), ununuaji na uuzaji wa fedha
za kigeni, uwekezaji katika hati fungani,(treasury bills & Bonds).
Ukusanyaji
wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni (cash management) pamoja na
ulipaji wa mishahara kwa Njia rahisi na haraka. Huduma zetu hutolewa kwa
umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha Mteja anafurahia mahusiano yake na
benki. Pia huduma ya Premier Banking kwa wateja wanaopenda kujitofautisha
zaidi” walieleza TIB.
Mkurugenzi wa Mkuu wa TIB Corporate Bank, Frank Nyabundege akizungumza
wakati wa Jukwaa la Biashara lililofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Regal
Naivera Jijini Tanga.
Waziri
wa Habari akiwa katika picha ya pamoja na wadau hao
Mkuu
wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano ya Benki ya TIB Corporate, Theresia Soka
akizungumza wakati wa Jukwaa hilo.
Waziri
wa Habari akiwa katika picha ya pamoja na wadau hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment