Mkuu wa Wilaya ameyazungumza hayo jana alipokuwa kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Msomera Kata ya Misima baada ya uongozi wa Kijiji hicho kuomba msaada wa kusikilizwa ili kuainishiwa mipaka baina ya Kata na Vijiji ili kuondoa muingiliano.
Mh. Gondwe alisema kuwa wataalamuwa ardhi watapima na kuonesha mipaka baina ya Halmashauri ya Mji na Wilaya ili wafahamu mipaka yao na kutambua wanapaswa kuitika wapi na kuondoa migongano inayokwamisha wananchi kushiriki katika maendeleo.
Alisema kuwa Msomera ni Kijiji kilichoanzishwa kisheria na kipo kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi hivyo wananchi wote wanapaswa kuheshimu na kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na kuwataka wananchi wote wanaokuja kwenye Kijiji hicho na maeneo mengine kufuata masharti ya maeneo husika kwani Tanazania ni huru kuishi kwa kila mwananchi isipokuwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
Aliongeza kuwa Kijiji cha Msomera kilitengwa maalumu kwa mifugo, wakulima ambao walikuwepo kabla ya kijiji hicho kupangwa kuwa kwaaajili ya mifugo watambuliwe na hawataondolewa, wakulima waliokuja baada ya kijiji kutambulika kuwa ni cha mifugo wataondolewa.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka wanakijiji cha Msomera kufuata utaratibu linapokuja suala la kuuza ardhi na kuingiza mifugo mipya kwa kushirikisha uongozi wa Kijiji na kufanya mikutano mikuu ya maamuzi ili kuwe na maaamuzi ya pamoja hata kama ardhi inayouzwa ni ya mtu binafsi.
“Kijiji kikipangiwa matumizi bora kitumike kama ilivyokusudiwa ili kuondoa migogoro, tunzeni ardhi yenu na rasilimali zenu kwa ustawi wa vizazi vyenu,haijalishi kama mnaleta ndugu zenu, taratibu lazima zifutwe kinyume na hapo sheria itachukua mkondo wake” amesema Mkuu wa Wilaya.
No comments:
Post a Comment