Bi. Hindu ajisalimisha kwa MO - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Sunday, December 10, 2017

Bi. Hindu ajisalimisha kwa MO



Kama unakumbuka, shabiki na mwanachama mkongwe wa Simba Chuma Suleiman maarufu kama Bi. Hindu alikuwa hataki kusikia kabisa habari za mambo ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ndani ya klabu yao hususan masuala ya hisa na kampuni.

December 3, 2017 MO alishinda kwa kishindo zabuni ya kuwekeza ndani ya Simba, baada ya MO kutangazwa mshindi na wanachama wengi waliohudhuria mkutano huo kuridhia, Bi Hindu alijitokeza na kwenda hadi MO kumpongeza.

Bi. Hindu amesema wapo watu watakaosema amevuta ‘mtonyo’ ili kukubali mabadiliko hayo ambayo yameridhiwa pia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) sambamba na serikali kupitia wizara inayosimamia masuala ya michezo.

“Kuna watu wanaweza wakasema nimepewa ‘kitita’ lakini mimi sipo huko, nipo katika kujenga Simba kwa sababu aibu inatukuta kila siku sisi mikono kichwani.”

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania Yazindua huduma ya mikopo isiyo na dhamana ili kukuza biashara za wafanyabiashara wadogo na wa kati

  Benki ya Absa Tanzania Yazindua huduma ya mikopo isiyo na dhamana ili kukuza biashara za wafanyabiashara wadogo na wa kati Benki ya Absa T...

Pages