Mwenyekiti UVCCM ashikiliwa na Takukuru - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Sunday, December 10, 2017

Mwenyekiti UVCCM ashikiliwa na Takukuru


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Dodoma inamshikilia Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Sadifa Juma Khamis kwa tuhuma za kugawa rushwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi.

UVCCM leo Jumapili Desemba 10, 2017 inachagua viongozi wapya wa ngazi ya Taifa watakaoongoza jumuiya hiyo ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano.

Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge, Zanzibar amekamatwa nyumbani kwake karibu na mnada wa zamani mkoani Dodoma.

Kamanda wa Takukuru mkoani Dodoma, Emma Kihanga amethibitisha kukamatwa kwa mwenyekiti huyo na kwamba watatoa taarifa zaidi baadaye.

"Ni kweli tumemkamata tangu jana usiku tumekesha tunafanya uchunguzi, nitatoa taarifa baadaye kuhusu tukio hilo," amesema.

Mkutano mkuu wa uchaguzi wa UVCCM unaendelea mjini Dodoma na miongoni mwa waliohudhuria ni Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akifunga mkutano mkuu wa uchaguzi wa Umoja wa Wanawake (UWT) jana Jumamosi Desemba 9, 2017 alisema hawajapokea malalamiko mengi kutoka umoja huo na kuzitaka jumuiya nyingine za CCM kujifunza UWT.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania Yazindua huduma ya mikopo isiyo na dhamana ili kukuza biashara za wafanyabiashara wadogo na wa kati

  Benki ya Absa Tanzania Yazindua huduma ya mikopo isiyo na dhamana ili kukuza biashara za wafanyabiashara wadogo na wa kati Benki ya Absa T...

Pages