ALIYEWAHIALIYEWAHI KUWA MKUU WA WILAYA SABA AZULUMIWA NYUMBA ,AMPIGIA MAGOTI RC MAKONDA - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Friday, February 2, 2018

ALIYEWAHIALIYEWAHI KUWA MKUU WA WILAYA SABA AZULUMIWA NYUMBA ,AMPIGIA MAGOTI RC MAKONDA







  Mzee Waziri akionesha hati halali ya umiliki wa nyumba hiyo pamoja na familia yake



Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya Saba hapa nchini adhulumiwa nyumba na mpangaji wake,baada ya kuuziwa na Mtu aliyetapeli nyumba hiyo. 


Akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya huyo mstaafu Waziri Juma amesema nyumba hiyo alikuwa akimpangisha mpangaji huyo ambaye Ni mchina,na alaikuwa akilipa kodi Kama ipasavyo lakini baada ya Muda akadai kuwa ameuziwa nyumba hiyo.

"Hii nyumba Ni kiinua mgongo changu na niliamua kuipangisha ili niweze kupata hela ya kunisaidia kimaisha katika wakati huu niliostaafu lakini nimedhulumiwa na mchina akidai ameinunua "amesema Juma Waziri. 

Aidha amebainisha kuwa kabla ya mpangaji huyo kuinunua nyumba hiyo ilikopwa fedha benki na Mtu asiyefahamika na walipofahamu walitoa taarifa kwa benki hiyo wasitoe mkopo huo lakini baadae ikaja onekana ilikopwa hela kwa nyumba hiyo kitu ambacho kiliwashangaza Sana 

Anaendelea kusema kuwa baada ya fedha hiyo kukopwa na Mtu asiyefahamika na ambaye Hakuna mwanafamilia alishindwa kurejesha mkopo huo,na kupelekea nyumba hiyo kuuzwa ili kulipa deni hilo la benki ndipo mpangaji huyo ambaye ni mchina aliinunua. 

"Mimi binafsi sijawahi kukopa benki wala kuuza nyumba maana hii nyumba inanisaidia kujikimu kipindi hiki cha uzeeni hivyo Naomba hawa walipfanya kitendo hiki waweze kuchukuliwa hatua."Amesema Juma. 

Kwa upande wa watoto wa Mzee huyo wamelaani kitendo hicho na kuomba wahusika kuchukuliwa hatua Kali za kisheria. 

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages