Friday, February 2, 2018
RC MAKONDA AONGEZA MUDA WA KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WANANCHI WAKE
Kutokana na idadi kubwa ya Wananchi waliojitokeza kupata msaada wa kisheria Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ameamua kuongeza siku moja hadi kesho ili kuhakikisha wananchi wote waliofika wanasikilizwa na kuhudumiwa.
RC Makonda pia amewatangazia Wananchi wote waliosikilizwa na wanasheria kufika ukumbi wa Diamond Jubilee ifikapo Tarehe 10 February kuanzia Saa moja Asubuhi kwaajili ya kupatiwa mrejesho.
Taarifa za kuongezwa kwa muda zimepokelewa kwa shangwe na Wananchi ambapo wamemsifu RC Makonda kwa kutanguliza Utu mbele kwa kuhakikisha wanyonge wanaipata haki yao waliyotaabika kuitafuta kwa miaka mingi.
HONGERA RC MAKONDA KWA KUTIMIZA NDOTO YA RAIS MAGUFULI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
APeF Yazindua Mfuko wa Ziada Kupanua wigo wa uwekaji Akiba, Uwekezaji na Ulinzi
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, akikabidhi waraka wa ofa kwa Kaimu Mwenyekiti ...
No comments:
Post a Comment