Tuesday, February 27, 2018
WAZIRI MWIJAGE AIPONGEZA DANUBE NA GSM KWAKUITIKIA WITO WA SERIKALI
Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM Farida Rubanza (kulia), akizungumza na wandishi wa habari katika hafla ya utiaji sahihi makubaliano kati ya kampuni hiyo na kampuni ya Danube Home inayojishughulisha na biashara ya kuuza samani ambapo kuptia makubaliano hayo watajenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza Samani za ndani katika eneo la Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Wanne kushoto ni Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage pamoja na maofisa wengine kutoka GSM na Danube.
Waziri wa , Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa pili kushoto), akizungumza katika hafla ya utiaji sahihi makubaliano kati ya kampuni za GSM na Danube Home inayojishughulisha na biashara ya kuuza samani ambapo kuptia makubaliano hayo watajenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza Samani za ndani katika eneo la Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kushotoni Mkurugenzi Mtendaji wa Danube Home, Sayed Habib, wapili kulia ni Rais wa Danube Home Tanzania, Ghalib Mohamed na Meneja Masoko wa GSM, Farida Rubanza. Hafla hiyo ilifanyika kwenye duka la Danube, Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Danube Home, Sayed Habib (katikati), akizungumza na wandishi wa habari katika ya utiaji sahihi makubaliano kati ya kampuni za GSM na Danube Home inayojishughulisha na biashara ya kuuza samani ambapo kuptia makubaliano hayo watajenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza samani za ndani katika eneo la Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa GSM, Fahad Ahmad pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ambae ndio alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage ambae ndio alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo akisalimiana na mmoja ya wawekezaji kwenye Kampuni ya Danube Home Raymond Healy, wengine ni Maofisa wa Kampuni hiyo.
Waziri wa Viwanda amezipongeza kampuni za GSM na DANUBE Kuweza kuungana na kutaka kuanzisha kiwanda kitakachotengeneza samani mbalimbali hapa nchini.
Waziri Mwaijage amezungumza leo katika tukio la makubaliano na kati ya kampuni zote mbili ambapo zimekubali kuungana na kuamua kutengeneza kiwanda kitakachozalisha samani mbalimbali ili kuwapa wananchi fursa ya kupata bidhaa kwa ukaribu na kwa bei nafuu .
Amesema serikali ipo tayari kuwatoa sapoti katika kuhakikicha kiwanda hicho cha kuzalisha samani kinakuwepo nchini ambapo amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho kuyapeleka watanzania kupata ajira na kusaidia kukuza uchumi wa viwanda.
"Nafahamu kyanzishwa kwa kiwanda hichi kwanza mmenisaidia mimi katika kutekeleza sera ya kukuza uchumi wa viwanda, pia itatengeneza ajira kwa wananchi wetu hivyo ni jambo jema na napenda kiwanda hichi kianzishwe" amesema Mwaijage.
Aidha amebainisha kuwa kutengenezwa kwa samani katika nchi yetu kitasaidia kukuza soko la biashara na wateja kupata bidhaa kwa bei nafuu na kwa urahisi zaidi.
Kwa upande wake Meneja masoko wa Kampuni ya GSM , Farida Rubanza amesema wana tarajia kujenga kiwanda kikubwa kitakacho kuwa kina tengeneza samani za ndani (Furniture) kwa ajili ya kuuza nchini na kusafirisha nchi mbalimbali duniani.
‘’Sisi GSM na DANUBE tumeona Nivema tukaungana ilikujenga kiwanda hapahahapa na tutakuwa tuna pata malighafi hapahapa na kiwanda kikikamilika tuta kuwa na uwezo wa kuuza Contener 500 kwa mwezi na tutauza masoko ya nje na ndani ‘’ alisema .
Rubanza pia ame mshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe. John P.Magufuli na serikali yake kwa kwa kuweka mazingira Rafiki kwa wawekezaji wa ndani na wa kigeni na kuahidi kuwa wao kama waekezaji wataendelea kutoa ajira kwa watanzania.
Katika muungano huu amesema, wataanzisha DUNUBE home Academy na watachukua wahitimu wa vyuo nchi na watawafundisha na kuwapatia ajira ndani na nje ya nchi walikowekeza na wemgine watawa tafutia ajira sehemu mbalimbali
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya DANUBE Home Sayed Habib amesema wamewiwa kuja kuwekeza Tanzania kwani ina rasilimali za kuweza kusaidia uzalishaji wa samani hizo.
Ameishukuru kampuni ya gsm kukubali kufanya muunganiko utakaosaidia kuanzishwa kwa kiwanda icho hapa nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...
No comments:
Post a Comment