Mfumuko wa bei Kitaifa kwa mwezi februari wapanda - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Thursday, March 8, 2018

Mfumuko wa bei Kitaifa kwa mwezi februari wapanda

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Februari, 2018 umeongezeka hadi kufikia asilimia 4.1 ikilinganishwa na asilimia 4.0 ilivyokuwa mwezi Januari, 2018.

Hii inamanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2018 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo, amesema “Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2018 kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei za bidhaa zisizo za vyakula ingawa kuna bidhaa chache za vyakula zilizochangia,”.

Ametaja baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei kati ya Februari, 2017 na Februari, 2018 ni pamoja na mkaa kwa asilimia 17.6, gesi ya kupikia kwa asilimia 11.1, mafuta ya taa kwa asilimia 9.9.

Bidhaa nyingine ni petrol kwa asilimia 13.1, dizeli kwa asilimia 11.3, huduma za meno kwa asilimia 21.9, viatu kwa asilimia 3.4, mavazi ya wanaume kwa asilimia 3.4 na mavazi ya wanawake kwa asilimia 3.8.

Akizungumzia hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki, Kwesigabo amesema nchini Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2018 umepungua hadi asilimia 2.1 kutoka asilimia 3.0 kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018.

Kwa upande wa Kenya amesema mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2018 umepungua hadi asilimia 4.46 kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2018.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania na ASA Microfinance Yaadhimisha Miaka Minne ya Mafanikio katika Kuwawezesha Wanawake na Kubadilisha Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa  Benki ya Absa  Tanzania, Bw.  Obedi Laiser  (Katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,...

Pages