RC MAKONDA AFANYA JAMBO HILI KWA WAMAMA WAJAWAZITO. - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Thursday, March 29, 2018

demo-image

RC MAKONDA AFANYA JAMBO HILI KWA WAMAMA WAJAWAZITO.

IMG_0400
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dk. Grace Maghembe, (kushoto), akikabidhi vifaa tiba  vya Mama mzazi kwaajili ya kujifungulia (Delivery Packs) kwa Mganga Mkuu wa Meno, wilaya ya Ubungo  Safaa Chunga, kwa niaba ya Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, hafla yamakabidhiano hayo imefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
IMG_0372
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dk. Grace Maghembe, akizungumza na waandishi wa habari kabla yakukabidhi vifaa hivyo


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametoa zawadi ya vifaa tiba vya Mama mzazi kwaajili ya kujifungulia (Delivery Packs) 200 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi million 20 Kama zawadi yake ya sikukuu ya pasaka kwa kinamama watakaojifungua kwenye msimu huu wa pasaka.

Gharama ya mfuko mmoja (package) ya Vifaa hivyo vya kisasa ni Shilingi laki Moja ambapo ndani yake kuna Mashuka, Vitambaa, Dawa, Mabomba ya Sindano, Pamba, Kibanio cha kitovu, Nyuzi, pedi za kinamama, Dawa ya kuzuia upotevu wa damu, Nyembe na Gloves ambapo vitatolewa Bure kwa Mama mzazi atakaejifungua msimu huu wa pasaka kwenye vituo vya Afya na zahanati zilizopo kwenye Wilaya Tano za Mkoa huo.

RC Makonda ametoa vifaa hivyo baada ya kubaini changamoto ya baadhi ya kinamama kushindwa kumudu gharama ya vifaa vya kujifungulia na kujikuta wanatumia kanga au nguo jambo ambalo ni hatari kiafya kwa mama na mtoto.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya RC Makonda kwa waganga wakuu wa halmashauri na wasimamizi wa vituo na Zahanati, Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Dr. Grace Maghembe amesema vifaa hivyo vitasaidia pia kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Vifaa hivi vinapatikana Bure kwenye Hospitali zote za Mkoa wa Dar es Salaam kwa Msimu huu wa Pasaka hivyo kwa wewe Mama unaetaka kujifungua fika Hospitalini vifaa vyako utavikuta.

KUTOA NI MOYO, SIO UTAJIRI.

No comments:

Post a Comment

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dk. Grace Maghembe, (kushoto), akikabidhi vifaa tiba  vya Mama mzazi kwaajili ya kujifungulia (Delivery Packs) kwa Mganga Mkuu wa Meno, wilaya ya Ubungo  Safaa Chunga, kwa niaba ya Mganga Mkuu wa wilaya hiyo,...

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *