RC MAKONDA AITAKA DAWASCO KUONGEZA JITIHADA KATIKA KUSAMBAZA MAJI - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Saturday, March 17, 2018

RC MAKONDA AITAKA DAWASCO KUONGEZA JITIHADA KATIKA KUSAMBAZA MAJI




Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Mhe. Paul Makonda  amelitaka Shirika la Maji Safi na Maji Taka  DAWASCO kuhakikisha linashughulikia  kero zote za maji  kwa Wananchi ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na kupatia ufumbuzi  tatizo la Maji Taka  yanayotiririka holela kwenye  makazi ya watu.


 Makonda ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa  Wiki ya Maji  ambapo amesema tatizo la  maji taka  limekuwa   kero sugu  katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo  jambo linalohatarisha hata Afya za wananchi.


Aidha  Mhe,  Makonda  ameitaka  DAWASCO  kuongeza jitihada za kufikisha huduma ya maji kwa wananchi ili kuenda sambamba na  sera ya Serikali ya awamu ya Tano ya kumtua mama ndoo kichwani.

Hata hivyo  Makonda  ametoa wito kwa watumishi wa  DAWASCO wanaokwenda kusoma mita  kwa wananchi kuwa na lugha nzuri  kwa wananchi pamoja na kushughulikia  kero ya wananchi kubambikiziwa kiwango kikubwa cha malipo ya bili za maji.

Kuhusu changamoto ya  upotevu wa maji Mhe, Makonda  amelitaka shirika hilo kulipatia majibu ya haraka tatizo hilo ili kiasi cha maji yanayopotea kiweze kuwahudumia wananchi.

Ili kufikisha huduma ya maji kwa  maeneo yenye changamoto RC Makonda  amejitolea kuchimba  visima 50  vya maji ambapo amewasihi Wenyeviti wa mitaa hiyo kuainisha maeneo ya  kuchimba visima hivyo.

Pamoja na hayo Makonda  ametaka uwepo wa  ushirikiano wa kikazi baina ya TANROAD, TANESCO, TARURA na DAWASCO  ili kumaliza changamoto ya kukatwa kwa miundombinu ya maji  wakati wa ujenzi wa barabara pamoja na  uharibifu wa barabar

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania na ASA Microfinance Yaadhimisha Miaka Minne ya Mafanikio katika Kuwawezesha Wanawake na Kubadilisha Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa  Benki ya Absa  Tanzania, Bw.  Obedi Laiser  (Katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,...

Pages