Wanawake wa Tanga Cement waadhimisha Siku ya Wanawake wakilipia bima ya afya kwa watoto na kutoa msaada wa magodoro kituo cha watoto wenye mazingira magumu - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Monday, March 12, 2018

Wanawake wa Tanga Cement waadhimisha Siku ya Wanawake wakilipia bima ya afya kwa watoto na kutoa msaada wa magodoro kituo cha watoto wenye mazingira magumu

Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Diana Malambugi, akishikana mikono na mlezi wa watoto katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia (Nyumba ya Furaha), Sista Irene Kafuka (kushoto) wakati akikabidhi msaada wa magodoro 20 ambapo pia walilipia  bima za afya ya NHIF  kwa watoto wote 46 wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kituoni hapo mjini Tanga jana.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia (Nyumba ya Furaha), wakibeba moja ya magodoro 20 waliyopewa msaada na Kampuni ya Tanga Cement katika hafla ambayo pia kampuni hiyo ililipa bima za afya ya NHIF  kwa watoto wote 46 wa kituo hicho kwa muda wa mwaka mmoja  ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kituoni hapo mjini Tanga jana. Katikati kushoto ni mlezi wa kituo, Sista Irene Kafuka na Meneja Rasilimali Watu wa Tanga Cement, Diana Malambugi.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Nancy Mkoyogo (kulia) akishikana mikono na mlezi wa watoto katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia (Nyumba ya Furaha), Sista Irene Kafuka (kushoto) wakati wakikabidhi msaada wa magodoro 20 pamoja na kulipia bima za afya ya NHIF  kwa watoto 46 wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya matukio ya wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kituoni hapo mjini Tanga jana.
Ofisa Masoko na Mawasiliano wa Tanga Cement, Hellen Maleko (kulia), akigawa chakula kwa watoto kituoni hapo jana katika hafla hiyo.
Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Diana Malambugi (wa pili kulia), akizungumza na baadhi ya  watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Casa Della Gioia (Nyumba ya Furaha), huku mlezi wa watoto kituoni hapo Sista Irene Kafuka (kulia), akiangalia.
Mmoja wa wafanyakazi wa Tanga Cement, Changwa Mjella, akisaidia kumlisha chakula mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho wakati wa tukio hilo.
Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho akionyesha umahiri wake wa kusakata muziki wa kizazi kipya katika hafla hiyo. (Picha zote na Mgongos Photography)


No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania na ASA Microfinance Yaadhimisha Miaka Minne ya Mafanikio katika Kuwawezesha Wanawake na Kubadilisha Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa  Benki ya Absa  Tanzania, Bw.  Obedi Laiser  (Katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,...

Pages