WATAALAM WAWASILISHA USANIFU WA AWALI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA MSALATO DODOMA - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Saturday, May 12, 2018

WATAALAM WAWASILISHA USANIFU WA AWALI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA MSALATO DODOMA

Meneja Mipango na Usanifu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mohamed Millanga (wa kwanza kushoto), akiangalia moja ya picha (hazionekani pichani) za usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliowasilishwa leo na Wahandisi Marrarchi Walis na Kamel Fazhani wa Kampuni ya Studi ya Tunisia kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo uliudhuriwa na wataalam mbalimbali wa usafiri wa anga.
Wahandisi Kamel Fazhani (kulia) na Marrarchi Walis (kushoto) wa Kampuni ya Studi ya Tunisia wakiwasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma leo katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), mbele ya wadau mbalimbali wa masuala ya usafiri wa anga.
Mhandisi Bernard Kavishe (aliyesimama) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), akichangia hoja katika mkutano uliofanyika leo wa uwasilishaji wa usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo umewasilishwa na wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia.
Mwonekano wa Jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma, uliowasilishwa leo katika usanifu wa awali kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na wataalamu kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia.
Said Mpwili wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) (nyuma aliyenyanyua mkono), akiwasilisha mapendekezo ya ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege kwa wataalam kutoka Kampuni ya Studi ya Tunisia, ambao leo katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wamewasilisha usanifu wa awali wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma.

No comments:

Post a Comment

APeF Yazindua Mfuko wa Ziada Kupanua wigo wa uwekaji Akiba, Uwekezaji na Ulinzi

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, akikabidhi waraka wa ofa kwa Kaimu Mwenyekiti ...

Pages