Shein aipongeza Benki ya NBC - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Tuesday, June 5, 2018

demo-image

Shein aipongeza Benki ya NBC

shein+nbc
Rais wa Zanzibar  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein (wa pili kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Theobald Sabi katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake mjini Zanzibari hivi karibuni.


Rais wa Zanzibar  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein ameipongeza Benki ya NBC kutokana na kasi yake na juhudi za kukuza uchumi wa Zanzibar.

Akizungumza kwa niaba ya rais wa Zanzibar katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo iliyofanyika mjini Zanzbar hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud amesema pato la taifa limekuwa likikuwa mwaka hadi mwaka kutokana na mchango unaotolewa na taasisi mbali mbali ikiwemo Benki ya NBC.

Aidha Dk.Shein ameihimiza benki hiyo kuendelea na juhudi zake za kuimarisha mazingira bora na huduma kwa wateja wake ili kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya huduma za kifedha yanayotokea siku hadi siku na kukuza maendeleo bora nchini.

Hata hivyo ameipongeza Benki hiyo kwa kuonesha umuhimu kwa wateja wake kwa kurejesha miongoni mwa faida wanazozipata ikiwemo kwa njia hiyo ya kufutarisha na kutoa huduma nyengine mbali mbali kwa jamii.

Awali akizungumza katika hafla hiyo ya futari Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC,  Dk. Kassim Hussein amesema kukuwa kwa huduma za kifedha Zanzibar pia kunatokana na huduma bora zinazotolewa na benki hiyo inayokwenda sambamba na mahitaji ya wateja wake.

Amesema mazingira salama yaliopo Zanzibar yanayoimarishwa na viongozi wakuu wa nchi imewezasha benki hiyo kufanya kazi zake za kutoa huduma za kifedha kwa ufanisi na umakini zaidi.

No comments:

Post a Comment

Rais wa Zanzibar  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein (wa pili kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Theobald Sabi katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa watej...

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *