Makamu ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka kampuni ya usambazaji na uuzaji wa gas ya Oryx Mohamed Mohamed (kushoto) alipotembelea banda hilo wakati wa
kuadhimisha wiki ya mazingira yaliyofanyika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
ORYX GAS “Rafiki wa Mazingira”
Dar es Salaam, June 2018; Katika kuadhimisha wiki ya mazingira mwaka huu nchini Tanzania kampuni mama katika usambazaji na uuzaji wa gesi ya ORYX ijulikanayo kama ORYX ENERGIES LTD imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na serikali ili kuhakikisha nishati mbadala inatumika badala ya mkaa ambao umeonekana kuwa na gharama kubwa sana.
ORYX GAS kwa nyakati tofauti wamekuwa wadau muhimu sana katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kutunza mazingira, na kwa muda mrefu wamekuwa na kampeni yao ya ORYX GAS “Rafiki wa Mazingira”. Katika kuhadhimisha wiki ya mazingira wameamua kuchukua fursa kujiunga na wadau wengine kushirikiana katika kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama nafuu sana ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa miti na mazingira kwa ujumla.
Akizungumza katika maonyesho hayo eneo la mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha mauzo kampuni ya gesi ya ORYX Bw. Jeffrey Nasser amesema kuwA; ORYX GAS amekuwa rafiki mkubwa sana wa mazingira pale tulipoamua kuwaletea nishati mbadala ya gesi, na haikuishia hapo tuu bali tuliwawezesha wananchi wengi sana nchi nzima kuipata kwa gharama ndogo na hata yale maeneo ya wananchi wa hali ya chini tumewawezesha kupata gesi yetu. Na Tunaamini tumeokoa miti mingi ambayo ingekatwa kwa matumizi ya kupikia.
Ili kuhakikisha kuwa watu wote wanatumia nishati ya gesi,kampuni ya ORYX imewekeza kwa kiwango kikubwa sana kwenye maghara ya uhifadhi na mitambo ya kujaza gesi nchi nzima.Hatutarajii kusikia tena uhaba wa gesi ya kupikia nchini na hatutarajii kabisa watumiaji wa gesi wanarejea kwenye mkaa na kuni kwa kukosa nishati hii ya gesi hapa nchini. Aliongezea Afisa Huyo wa ORYX .
Akielezea kaulimbiu ya mwaka huu ya Mkaa ni gharama sana; Bwana Bw. Jeffrey amesema kuwa Mkaa ni gharama sana hasa kwa wakazi wa mijini. Sasa hivi gunia la mkaa kwa wakazi wa Dar es salaml imefikia shilingi 70,000 na wengi wanalalamika kuwa mkaa haumalizi mwezi.Sisi tunawapa mtungi wa gesi wa kilo 15 ambao kwa familia ya watu saba wanaotumia gesi pekee huweza kutumia kati ya siku 30 hadi 40. Mbali na faida za gharama ndogo,gesi yetu pia ni salama kwa afya ya mtumiaji na usafi wa mazingira ambapo tusingeanza usambazaji mkubwa wananchi wangepaswa kuweka bajeti nyingine za matibabu ya madhara ya moshi mwilini na ukarabati wa nyumba ambazo huchafuka sana kutokana na matumizi ya kuni na mkaa.
Kampuni ya ORYX imetoa shukurani sana kwa wananchi kwa muitikio mkubwa sana wa matumizi ya gesi kila siku inayoenda. Muitikio mkubwa umeonekana hasa pale ongezeko la watumiaji wengi wapya nchi nzima wakinunua mitungi mipya ya gesi ya ORYX kwa matumizi yao. Mbali na hapo wengiwamerudisha mrejesho kuwa walichelewa kuanza kutumia ges hiyo na wamehuakikishia uongozi wa kampuni ya ORYX kuwa hawatarudi tena kutumia kuni na Mkaa.
Kampuni ya ORYX inatoa wito kwa jamii yote kwenda na mabadiliko ya matumizi ya nishati ya kupikia, Oryx Gas kama wasambazaji wakubwa sana nchini wameona muitikio mkubwa sana kwa jamii mbalimbali nchi nzima hususani pembezoni mwa nchi.
Kampuni ya ORYX pia wametoa wito kwa serikali kuzidi kushirikiana nao katika kuhamasisha wananchi katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati mbadala ya gesi. Na pia wameiomba serikali kusimamia Sheria za mazingira kwa ukamilifu ili watu waelewe na waone umuhimu wa kutunza misitu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
No comments:
Post a Comment