RC MAKONDA Atimiza Ahadi ya Kuwalipia Ada ya Kidato Cha Tano na Sita kwa Watoto wa Kike 100 Kutoka Familia Duni Waliofaulu Masomo ya Sayansi na Kushindwa kuendelea na Masomo kwa kukosa Ada. - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Tuesday, September 17, 2019

RC MAKONDA Atimiza Ahadi ya Kuwalipia Ada ya Kidato Cha Tano na Sita kwa Watoto wa Kike 100 Kutoka Familia Duni Waliofaulu Masomo ya Sayansi na Kushindwa kuendelea na Masomo kwa kukosa Ada.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimkabidhi bahasha yenye hundi ya malipo ya Ada ya shule na matumizi ya msingi kwaajili ya masomo yake, kwa mmoja wa wanafunzi aliyenufaika ufadhili huo, (kulia) Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Bw. Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wanufaika wa ufadhili wa kulipiwa Ada ya Kidato Cha Tano na Sita kwa Watoto wa Kike 100 Kutoka Familia Duni Waliofaulu Masomo ya Sayansi na Kushindwa kuendelea na Masomo kwa kukosa Ada.
Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Bw. Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi akimkabidhi bahasha yenye hundi ya malipo ya Ada ya shule na matumizi ya msingi kwaajili ya masomo yake, kwa mmoja wa wanafunzi aliyenufaika ufadhili huo.
Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Bw. Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi akimkabidhi bahasha yenye hundi ya malipo ya Ada ya shule na matumizi ya msingi kwaajili ya masomo yake, kwa mmoja wa mzazizi wa mwanafunzi aliyenufaika ufadhili huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wanufaika wa ufadhili wa kulipiwa Ada ya Kidato Cha Tano na Sita kwa Watoto wa Kike 100 Kutoka Familia Duni Waliofaulu Masomo ya Sayansi na Kushindwa kuendelea na Masomo kwa kukosa Ada.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda September 17 ametimiza ahadi ya ufadhili wa Masomo kuanzia Kidato cha Tano hadi Sita kwa Watoto wa kike 100 kutoka familia duni waliofaulu masomo ya Sayansi lakini wakashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa Ada ambapo katika ufadhili huo amewalipia Ada na Vifaa ya shule ikiwemo Sare, mabegi, vitabu, madaftari na Nauli.

RC Makonda amesema lengo la ufadhili huo ni kumkomboa mtoto wa Kike kutoka familia duni aweze kupata elimu bora itakayosaidia kubadili maisha ya Familia na mwisho wa siku kuwa na Taifa lenye Wanawake Wanasayansi na Wagunduzi.

Aidha RC Makonda amesema ufadhili huo unaenda sambamba pia na kumuunga Mkono Rais Dkt.John Magufuli alieamua kumkomboa mtoto wa mnyonge kwa kutoa elimu bure kuanzia Darasa la Kwanza hadi kidato cha nne na yeye ameamua kupokea kijiti kwa kuwasomesha kidato cha tano na Sita ili wakifika vyuo vikuu wanufaike na Mkopo.

Hata hivyo RC Makonda amesema zoezi hilo litakuwa endelevu kila mwaka ambapo amewahimiza wanafunzi waliobahatika kupata fursa hiyo waitumie vizuri huku akimshukuru Balozi kwa Kumuunga mkono katika kampeni hiyo.




Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Bw. Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi amesema ufadhili huo ni Mwendelezo wa Kuunga Mkono juhudi za RC Makonda kwenye kila jambo kwakuwa amekuwa mtu wa kupigania maslahi ya Wananchi anaowaongoza.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa yaendeleza udhamini wake Absa Dar City Marathon

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga (wa pili kushoto) akionyesha fulana zitakazovaliwa siku ya mbio ...

Pages