Sunday, October 27, 2019
Benki ya DCB yadhamini Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania
Waziri katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, Suleiman Jaffo, akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), kwa kutambua udhamini
wa benki hiyo katika hafla ya kutoa Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa
wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa waliofanya vizuri katika
mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki.
Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Godfrey Mweli.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa,
Joseph Kandege (kulia), akishiakana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa baara ya kupokea cheti cha shukurani kutoka
kwa Waziri wa Tamisemi, kutoka na udhamini wa benki hiyo katika hafla ya kutoa
tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri
na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika
jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya Biashara ya DCB,
Fredrick Mwakitwange (kushoto), akimfahamisha Angel Lomwai kuhusu faida ya
akaunti maalumu ya mpango wa elimu ya ‘DCB Skonga’ iliyozinduliwa na benki hiyo
hivi karibuni wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa
wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa waliofanya vizuri katika
mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki.
Ofisa Mahusiano wa Benki ya Biashara ya DCB, Dalila Issa (wa
pili kushoto), akitoa maelezo kuhusu akaunti maalumu ya masuala ya elimu
ya DCB Skonga iliyozinduliwa na benki hiyo hivi karibuni wakati hafla ya utoaji
tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule,
halmashauri na mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka
2019 iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya utoaji tuzo za Ubora
wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na mikoa
waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini Dar
es Salaam mwisho mwa wiki ambayo DCB iliidhamini.
Baadhi ya wahudhuriaji katika hafla ya utoaji tuzo za
Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na
mikoa waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 iliyofanyika jijini
Dar es Salaam mwisho mwa wiki ambayo DCB iliidhamini wakifuatilia matukio
mbalimbali ya utoaji tuzo hizo.
BENKI
ya Biashara ya DCB itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya
tano katika kuleta maendeleo ya elimu
nchini huku ikileta bidhaa na huduma maalumu za kielimu zinazolenga kuhakikisha
watoto wa kitanzania wanapata elimu bora kwa mustakabali wa maendeleo yao
binafsi na kwa taifa.
Akizungumza
katika hafla ya kutoa Tuzo za Ubora wa Elimu Tanzania kwa wanafunzi, walimu,
shule, halmashauri na mikoa waliofanya
vizuri katika mitihani ya taifa mwaka 2019 jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki ambazo DCB ilidhamini, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema DCB inatambua juhudi kubwa inayofanywa
na Rais John Joseph Pombe Magufuli katika kuboresha na kuinua kiwango cha elimu
nchini, juhudi zilizoanza kujionyesha mwanzo kabisa pale alipoondoa ada za
shule kuanzia elimu ya msingi hadi Sekondari.
“Kwa
kutambua umuhimu wa elimu Benki ya DCB hivi karibuni tulizindua akaunti maalumu
iitwayo ‘DCB Skonga’ ikilenga kumsaidia mteja wetu kuweka akiba kidogo kidogo
huku tukimpa uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi kufikia chuo kikuu.
“Kumekuwa na changamoto kubwa sana katika jamii inayotuzunguka
pindi mzazi/mlezi anaetegemewa na familia anapopoteza maisha au kupatwa na ulemavu
wa kudumu, kwani watoto wengi wanashindwa kuendelea na masomo hii imetengeneza
hofu kwenye familia nyingi. Kutokana na changamoto hizo, DCB tulianzisha bidhaa
hii maalum ya mpango wa elimu inayomuwezesha mtoto kusoma hadi kumaliza elimu
ya chuo kikuu bila ya shida yoyote”, aliongeza mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi huyo alisema akaunti hiyo inampa fursa mteja kuchagua
muda wa kuweka akiba kuanzia mwaka 1
hadi 17 na endapo atapoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu kabla ya muda
kwisha, mtegemezi hurudishiwa kiasi cha
fedha alichoweka kuanzia mwanzo wa mpango na vilevile mtoto atalipiwa gharama
zote za elimu pamoja na hela ya matumizi ya shule kwa kipindi chote
kilichosalia cha mkataba.
Kuhusu
maendeleo ya benki Bwana Ndalahwa alisema DCB imeweka kipaumbele katika
kusaidia jamii hususani kwenye utoaji wa elimu na mitaji midogo midogo kwa
wananchi wa kipato cha chini ambapo hadi mwishoni mwa Disemba 2018 imeweza
kutoa mikopo yenye jumla ya shilingi bilioni 160 kwa wafanyabiashara wadogo wa
vikundi ikiwemo shilingi bilioni 16 zilizotolewa kwa mfuko wa wanawake na
vijana wa halmashauri za Jiji la Dar es Salaam kupitia njia ya ukopeshaji wa
vikundi vidogo.
“Mikopo
hii yenye masharti na riba nafuu imeleta chachu katika kuendeleza jamii kwani
imewasaidia wazazi kufanya biashara na kusomesha watoto wao. Benki imetoa
mikopo kwa zaidi ya watanzania 38,000 ambao wananufaika na huduma hizi. DCB pia
ndio benki ya kwanza kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali na kupitia mikopo
hii wafanyakazi hawa wameweza kuimarisha maisha yao”, alisema.
Pamoja
na mikopo hiyo alisema DCB pia imeendelea kutoa mikopo ya nyumba za bei nafuu
kwa watanzania ambao maeneo yao hayajapimwa na wanaamini kupitia mikopo hii pia
wazazi wameweza kujenga nyumba zao na kusomesha watoto, yote hiyo ikiwa ni
katika kuunga mkono serikali ya awamu ya
tano ya kuhakikisha watanzania wanaishi maisha bora.
“Benki ya DCB itaendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali
wa elimu katika mambo yenye kuleta maendeleo ya sekta za elimu nchini na
tungependa kutoa pongezi zetu kwa wanafunzi, walimu, shule, halmashauri na
mikoa iliyofanya vizuri katika mitihani ya taifa kwani washahili walisema
‘Mcheza kwao hutunzwa’ na leo tunawatunza”, alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Biashara DCB kuendelea kuboresha Maisha ya Watanzania
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bias...
No comments:
Post a Comment