RC MAKONDA AWATAKA TBA KUKAMILISHA UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA UBUNGO KABLA YA DISEMBA 30 MWAKA HUU - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Monday, October 7, 2019

RC MAKONDA AWATAKA TBA KUKAMILISHA UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA UBUNGO KABLA YA DISEMBA 30 MWAKA HUU


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka Wakala wa Majengo Tanzania TBA kuhakikisha ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo unakamilika na kuanza kutumika kabla ya Disemba 30 Mwaka huu likiwa Viwango na Ubora unaotakiwa.

RC Makonda amechukizwa kuona mkataba wa ujenzi huo umesainiwa tokea Disemba 13 mwaka jana na kazi inatakiwa kukamilika Disemba 13 mwaka huu lakini hadi sasa ujenzi umefikia 35% huku muda wa mkandarasi kuwa site ukiwa mkubwa kuliko kazi aliyoifanya.

Kilichomkwaza zaidi RC Makonda ni kubaini kuwa ujenzi ulisimama kwa zaidi ya Miezi miwili kwa kigezo cha Manispaa kuchelewa kutoa fedha huku muhusika akikaa kimya pasipo kutoa taarifa kwenye ngazi ya Mkoa ili mkoa uweze kuingilia kati fedha itoke kwa wakati.

Aidha RC Makonda amefanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la Kisasa la Juu (Interchange) Ubungo ambapo ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo na kumuelekeza mkandarasi kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.

Pamoja na hayo RC Makonda pia amefanya ziara ya Ukaguzi wa Maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha na kueleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo.

Katika ziara hiyo RC Makonda ametembelea Ujenzi wa Kituo cha Afya Kimara na kumuelekeza Katibu tawala wa Mkoa huo kutuma timu ya kufuatilia upya ujenzi wa Jengo la gorofa katika kituo hicho linalogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2 baada ya kubaini gharama za ujenzi ni kubwa kuliko idadi ya majengo wakati Wilaya ya Kigamboni imetumia Bilioni 1.5 kujenga majengo saba ya kisasa.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Biashara DCB kuendelea kuboresha Maisha ya Watanzania

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bias...

Pages