RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI - THINKING IN BUSINESS

Mgongopr.blogspot.com is a business centered online platform highlighting trade, finance and economic news in Tanzania. Our coverage is customised to ensure we consolidate brands, boost sales and nurture investments. The site is an imprint of Mgongo Logistics and Solutions, a trusted consultancy firm, offering Social Media Management, Photography, Videography, Advertising, Event Management and Translation. For more information contact us via; Phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, October 9, 2019

RC MAKONDA AZINDUA MFUMO WA KUWEZESHA WANANCHI KUTOA MALALAMIKO DHIDI YA WATENDAJI WASIOTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda October 09 amezindua Mfumo wa kuwawezesha wananchi wa Mkoa huo kuwasilisha kero na changamoto walizonazo kwa kutumia simu ya mkononi au Computer na ujumbe wao kuwafikia watendaji kwa haraka na kupatiwa majibu ndani ya muda mfupi jambo litakalosaidia kuokoa Muda na gharama za usafiri.

RC Makonda amesema ameamua kuanzisha mfumo huo baada ya kubaini kuwa wananchi wengi wamekuwa wakifika kwenye ofisi za umma na kupewa majibu ya "Njoo Kesho" pasipokujua kuwa wamepoteza muda na nauli zao kufuata huduma.

Aidha RC Makonda amebainisha kuwa mfumo huo utakuwa ukipokea taarifa za malalamiko ya Watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata, Wilaya hadi Mkoa na taarifa zitawafikia Viongozi wote kuanzia RC Makonda mwenyewe, Mkuu wa Wilaya husika, Mkurugenzi, Katibu tawala na Mkuu wa idara.

Hata RC Makonda amewahimiza wananchi kutumia mfumo huo kueleza kero zote zinazowakabili ikiwemo Afya, Barabara, Elimu, Maji, Umeme, Miradi inayokwama pamoja na kutoa taarifa pindi wanapobaini uhalifu kwenye mtaa.

Jinsi kuwasilisha ujumbe andika neno DSM kisha eleza changamoto zako kisha tuma kwenye namba 11000 au ingia kwenye Website www.malalamiko.dsm.go.tz na ujumbe wako utapokelewa mara moja na kupewa mrejesho.

HUDUMA HII NI BURE.

No comments:

Post a Comment

SERIKALI YASISITIZA UTAALAMU NA UBUNIFU KATIKA UNUNUZI NA UGAVI

Serikali imewataka wataalam wa ununuzi na ugavi nchini kuongeza ubunifu, uongozi bora na matumizi ya teknolojia za kisasa ili kuongeza ufani...

Pages