Thursday, October 24, 2019
Home
LOCAL
WAKANDARASI WALIOLETA "JANJAJANJA" MIRADI YA UJENZI DAR WAKAMATWA NA POLISI KWA AGIZO LA RC MAKONDA
WAKANDARASI WALIOLETA "JANJAJANJA" MIRADI YA UJENZI DAR WAKAMATWA NA POLISI KWA AGIZO LA RC MAKONDA
Wakandarasi wa Kampuni za
CHICCO Engineering na Nyanza Road Work leo wamekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda
maalumu ya Dar es salaam kwa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul
Makonda ambae ameagiza kukamatwa kwa wakandarasi hao kwa kosa la Kushindwa
kutekeleza miradi ya Ujenzi wa Mto Ng'ombe na Barabara ya Kivule kwa wakati na
kuleta usumbufu Mkubwa kwa wananchi ukiwemo wa Mafuriko, Nyumba Kubomoka,
Uharibifu wa Mali, Ajali na Magari kuharibika huku wakandarasi hao wakila
Maisha mitaani.
Kwa mujibu wa RC Makonda
Mkandarasi wa Kampuni ya CHICCO
amekamatwa kwa kushindwa kuanza Mradi wa ujenzi wa Mto Ng'ombe unaogharimu
Shilingi Bilioni 32 ambapo licha ya Kusaini Mkataba Mkandarasi huyo hajaanza
kazi kwa zaidi ya Miezi minne na hadi sasa amelipwa zaidi ya Shilingi Bilioni
4.8 huku wananchi wakiteseka na kero ya Mafuriko.
RC Makonda amesema jambo hilo
ni uzembe na hujuma inayoweza kuchonganisha Wananchi na Serikali yao ambayo
tayari imetoa fedha za ujenzi wa Mto huo ili kuwaondolea kero lakini Mkandarasi
amekuwa akisuasua kuanza kazi.
Kwa upande wa Kampuni ya Nyanza
RC Makonda ameagizwa kukamatwa kwa Mkandarasi huyo kwa kushindwa kukamilisha
ujenzi wa Barabara ya Kivule na Daraja licha ya Kupokea fedha zaidi ya Shilingi
Milioni 800 jambo linalopelekea wakazi wa Kivule kuteseka na kero ya ubovu wa
Barabara na wakati mwingine kusababisha Ajali na Kuharibika kwa Vyombo vya
usafiri.
Kwa Maelekezo ya RC Makonda
Wakandarasi hao waliokamatwa watakuwa Wakilala Polisi Central na asubuhi
watatokea polisi kwenda kufanya kazi ya Ujenzi hadi hapo atakapojiridhisha kuwa
kazi inaenda vizuri huku akieleza kuwa zoezi hilo la ukamataji litakuwa
endelevu kwa Wakandarasi wote wanaokwamisha miradi ya serikali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Biashara DCB kuendelea kuboresha Maisha ya Watanzania
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bias...
No comments:
Post a Comment