Tuesday, November 12, 2019
Wateja watano wajishindia bodaboda na Ibuka Kidedea na NBC Malengo
Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Alina
Maria Kimaryo (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es
Salaam leo wakati NBC ikichezesha droo ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya
Malengo ambapo wateja watano walijishindia zawadi ya bodaboda kila
mmoja. Wengine pichani ni maofisa wa benki hiyo na kulia kabisa ni
mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha.
Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Alina
Maria Kimaryo (mbele kulia), akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati NBC
ikichezesha droo ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC ambapo
wateja watano walijishindia zawadi ya pikipiki aina ya Yamaha kila
mmoja. Washindi wa leo ni; Augustine Hatari kutoka Pwani,
Williumu Pendaeli Isack wa Moshi, Scholastica Peter Yamawasa, Honest
Christopher Kimaro na Daudi Majani wote kutoka Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam,
WATEJA
Watano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wameibuka washindi wa bodaboda mpya
aina ya Yamaha katika droo ya kwanza ya kampeni ya “IBUKA KIDEDEA NA NBC”
kupitia akaunti ya Malengo ya benki hiyo kongwe hapa nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwenye droo ya kwanza ya
kampeni hiyo iliyoanza mwezi wa Oktoba, Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina
Maria Kimaryo alisema kwamba akaunti ya malengo inampa mteja njia rahisi ya
kuweka akiba kidogo na kupata faida kubwa kila mwezi.
“kwenye
akaunti hii ya malengo kila Tsh 100,000 atakayoweka mteja kwenye akaunti hii
inampa nafasi ya kushida zawadi kemkem ikiwemo bodaboda ambapo leo droo ya
kwanza itashuhudia wateja hawa watano wakipata zawadi zao,” alisema Kimaryo.
Aliongeza
kwamba katika kipindi chote cha kampeni bodaboda tano aina ya Yamaha zitatolewa
kila mwezi na safari tatu za kwenda kufanya utalii Serengeti na safari tano za
kwenda Seychelles mwezi wa Disemba na washindi wanaruhusiwa kwenda na mtu mmoja
kwenye safari hizo.
“ukiwa
na akaunti ya NBC malengo unapata faida nyingi ikiwemo ya kuhifadhi fedha kwa
ajili ya kutimiza malengo na ndoto zako pamoja na mambo mengine ya kupata riba
ya hadi asilimia 7 ya pesa uliyoweka kila mwezi,’ alisisitiza Kimaryo.
Washindi
kwenye droo ya jana walikuwa ni Augustine Hatari kutoka Pwani, Daudi Majani,
Dar es Salaam, Williumu Pendaeli Isack, Moshi Kibololoni, Scholastica Peter
Yamawasa, Dar es Salaam, na Honest Christopher Kimaro wa Dar es Salaam.
Katika
kampeni hii wateja watakao ongeza salio kwa kiasi Tsh milioni moja kwenye
akaunti ya Malengo watapata nafasi ya kushinda zawadi kuu ya TOYO na jumla ya
TOYO tatu zitatolewa kwenye kampeni hiyo ya “IBUKA KIDEDEA NA NBC MALENGO”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Biashara DCB kuendelea kuboresha Maisha ya Watanzania
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa nne kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Bias...
No comments:
Post a Comment