Saturday, December 21, 2019
Home
BUSINESS
NBC yazindua Kampeni ya Bima ya magari kipindi hiki cha sikukuu kwa kushirikiana na SANLAM
NBC yazindua Kampeni ya Bima ya magari kipindi hiki cha sikukuu kwa kushirikiana na SANLAM
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki
Masuke (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari
inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho
wa mwaka. Kampeni iliyozinduliwa na NBC kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam
imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam
jana. Kutoka kushoto ni; Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin Nkaka, Meneja Masoko wa
Sanlam, Marco Yambi na Mkurugenzi wa Mauzo wa Total, Marieme Sow.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki
Masuke (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Mauzo wa Total, Marieme Sow (kushoto
kwake), wakionyesha kadi ya kuwekea mafuta ya Total wakati wa uzinduzi wa
kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika
msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayofanyika kwa kushirikiana
na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi,
jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni; Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin
Nkaka, Meneja Masoko wa Sanlam, Marco Yambi, Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano
wa Total, Marsha Msuya na Meneja Mahusiano Kitengo cha Bima cha NBC, Kuruthum
Mwaluwinga.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki
Masuke (kushoto), akikabidhi kadi ya kujazia mafuta ya Total kwa mteja wa
kwanza kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Danford
Robert Buguru wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga
zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.
Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa
katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana.
Wanaoangalia ni wawakilishi kutoka NBC, Sanlam na Total.
Mkuu wa Kitengo cha Bima cha Benki ya NBC,
Benjamin Nkaka (kushoto), akikabidhi zawadi mbaimbali kwa mteja wa kwanza
kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Robert Danford
Buguru, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari inayowalenga zaidi
watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni
hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika
kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoangalia ni
wawakilishi kutoka NBC, Sanlam na Total.
Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki
Masuke (katikati), akisaidia kuweka mafuta ya ofa katika gari la mteja wa
kwanza kukata bima ya gari kupitia huduma za bima za NBC na Sanlam, Robert
Danford Buguru (kulia), wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bima ya magari
inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa sikukuu za mwisho
wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Sanlam
imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini Dar es Salaam
jana. Nyuma yake ni Mkuu wa Bima wa NBC, Benjamin Nkaka.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa Benki ya NBC, David
Raymond (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ambapo NBC ilizindua kampeni
ya bima ya magari inayowalenga zaidi watumia vyombo vya usafiri katika msimu wa
sikukuu za mwisho wa mwaka. Kampeni hiyo inayoendeshwa kwa kushirikiana na
Kampuni ya Sanlam imezinduliwa katika kituo cha mafuta cha Total, Mbezi, jijini
Dar es Salaam jana.
Benki
ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Sanlam imezindua
kampeni ya bima ya magari itakayojulikana kama “Ifurahishe gari yako”.
Kampeni
hiyo inayoanza Desemba mwaka huu hadi Januari mwakani ni sehemu ya malengo ya
benki kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja kwa kuwapa mahitaji muhimu
kupitia huduma bora zilizoandaliwa mahsusi kwa ajili yao.
Kwa
kutambua umuhimu wa usalama kwa wasafiri na watumiaji wote wa vyombo vya moto
kwa ujumla, katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, NBC imemrahisishia mteja
kupata kifurushi kizuri cha bima kwa ajili ya magari kikiambatana na nyongeza
kadhaa za kuvutia.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Kituo cha Mafuta cha Total, Mbezi
jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Bima wa NBC, Benjamin Nkaka alisema
kampeni hiyo imezinduliwa katika kipindi sahihi cha mwaka ambapo kwa kawaida
huwa na idadi kubwa ya wasafiri.
NBC
imedhamiria kuboresha huduma za bima na kufanya kasi ya matumizi ya bima nchini
kuongezeka, kwa kupitia kampeni hii, wateja watakaonunua bima katika matawi ya NBC
watapata ofa kadha wa kadha zikiwemo huduma ya bure ya mafuta ya kilainishi cha
injini na mafuta ya bure kutoka vituo vya mafuta vya Total pamoja na bima ya
bure ya ajali ulemavu wa kudumu na gharama za matibabu kutokana na ajali.
Akifafanua
zaidi kuhusu kampeni hiyo, Meneja Mahusiano wa Bima kutoka NBC Bi. Kuruthum
Mwaluwinga alisema, wamiliki wa magari yenye thamani ya TZS 50,000,000 na zaidi
watanufaika na mafuta bure pamoja na bima ya bure ya ajali, ulemavu wa kudumu
na gharama za matibabu kutokana na ajali.
Aliongeza
kuwa kwa wateja wenye magari yenye thamani ya kuanzia TZS 15,000,000 hadi 49,900,000,
watapata lita 10 za mafuta bure katika kituo chochote cha Total nchi nzima, bima
ya ajali ama ulemavu wa kudumu na gharama za matibabu.
Mwisho,
kwa wateja wenye magari yenye thamani ya kuanzia TZS 7,000,000 hadi 14,900,000,
watapata lita tano za bure za mafuta katika kituo chochote cha Total nchini,
bima ya ajali ya bure ama ulemavu wa kudumu na gharma za matibabu. Wateja wote kwenye
vipengele tajwa watapata kadi ya Total kwa ajili ya kujazia mafuta.
Alimaliza
kwa kusema: "NBC kupitia Sanlam na kampuni nyingine za bima hutoa huduma
bora za bima za aina mbalimbali kwa wateja wetu zikijumuisha bima za maisha na
za kawaida. Huduma hizi tayari zipo katika matawi yetu yote yanayopatikana kote
nchini.”
Kwa upande
wake, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Binafsi
wa NBC, Elibariki Masuke, alisema kuzinduliwa kwa kampeni hiyo ni ishara wazi
ya dhamira NBC kutoa huduma bora za kifedha
kwa wateja wake hapa Tanzania.
"Pamoja
na uzoefu wa zaidi ya miaka 50 ya kutoa huduma za kuvutia, siku zote NBC inajivunia
kuzindua huduma zenye viwango vya juu kwa manufaa ya wateja wetu. Tunawakaribisha
wote kutumia na kufurahia huduma hizo za kibenki.”
NBC
imeendelea kuwa kinara katika ubunifu ambapo kwa mwaka huu pekee imefanikiwa
kuzindua huduma na bidhaa kadhaa za kufurahisha, kama Klabu ya Biashara ya NBC inayolenga
kuwapa maarifa muhimu ya biashara wafanyabiashara wa kati na wadogowadogo ili
waweze kuendeleza biashara zao kwa ufanisi; NBC
Kiganjani ambayo ni suluhisho rahisi kwa watumiaji kwani ni huduma za
kidijitali zinazotembea. Bidhaa nyingine mpya ni Akaunti ya Fasta inayowezesha
kufunguliwa kwa akaunti haraka na mteja kupewa kadi ya Visa papo hapo.
Kwa
muktadha huo huo, NBC imeendelea kukuza mtandao wa mawakala wa huduma zake (NBC
Wakala) nchini. Zaidi ya mawakala 2,200 wanawezesha huduma za kibenki
kupatikana kwa urahisi hata katika maeneo pasipokuwa na matawi ya benki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ABSA BANK TANZANIA SEES GLOBAL VOLATILITY AS A CATALYST FOR TANZANIAN COMPETITIVE ADVANTAGE
Corporate Banking Director at Absa Bank Tanzania, Ms. Nellyana Mmanyi, addresses participants during a meeting organized for senior business...
No comments:
Post a Comment