Monday, January 27, 2020

NBC yawataka wanawake wajasiriamali kujiunga na klabu ya biashara ya benki hiyo
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Uwekezaji, Angela Kairuki,
(wa pili kushoto) akishikana mikono na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja
Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri wakati wa semina ya kwanza ya wanawake wa
Kiislam kuhusu Ujasiliamali na Tanzania ya Viwanda iliyofanyika katika
Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na waalikwa wengine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki (wa pili kushoto), akishikana mikono na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja
Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri wakati wa semina ya kwanza ya wanawake wa
Kiislam kuhusu Ujasiliamali na Tanzania ya Viwanda iliyofanyika katika
Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Weningine
kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi la NBC
Corporate, Mariam Kombo, Meneja wa Tawi la NBC samora Zubeider Haroun, pamoja
na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya semina hiyo, Mariamu Dedes.
Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri,
akizungumza na Wanawake wajasiliamali wakati Warsha ya kwanza ya wanawake wa
Kiislam kuhusu Ujasiliamali na
Tanzania ya Viwanda iliyodhaminiwa na Benki ya NBC na kufanyika katika Ukumbi
wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Mgeni rasmi
katika semina hiyo alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela
Kairuki akimwakilisha Makamu wa Raisi, Mama Samia suluhu Hassan.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki (katikati), akipunga mkono
wakati akiondoka katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam juzi, baada ya
kufungua semina ya kwanza ya wanawake wa
Kiislam kuhusu Ujasiliamali na Tanzania ya Viwanda iliyodhaminiwa na Benki ya
NBC. Kushoto ni Naibu waziri wa zamani na mmoja wa viongozi wa wanawake wa
kiislamu katika Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mama Shamin Khan
pamoja na wahudhuriaji wengine.
Baadhi ya Washiriki wakiwa katika semina hiyo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam juzi. Semina hiyo ilidhaminiwa na Benki ya NBC. (Picha zote na Brian Peter)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa kuendelea kuunga mkono maendeleo ya wanawake mahali pa kazi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto), akikabidhi cheti Kwa Mkurugenz...

No comments:
Post a Comment