Thursday, January 9, 2020
Wateja watano wa NBC washinda Yamaha, Ibuka Kidedea na NBC Malengo
Meneja wa Kampeni ya Ibuka
Kidedea na NBC Malengo, Mtenya Cheya (kushoto),
akizungumza na mmoja washindi aliyeshinda zawadi ya bodaboda katika droo ya
tatu ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake
ni Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza wa NBC, Dorothea Mabonye, Meneja Chapa na
Mawasiliano wa benki hiyo, David Raymond na Wakaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha, Elibariki Sengasenga na Abdallah Hemedi.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa Benki ya NBC, David Raymond (wa tatu kushoto), akizungumza waandishi wa habari katika
droo ya tatu ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo jijini Dar es Salaam
leo. Kutoka kushoto ni; Meneja wa kampeni hiyo, Mtenya Cheya, Meneja wa Bidhaa
za Kuwekeza wa NBC, Dorothea Mabonye, na mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha, Elibariki Sengasenga.
Maofisa wa NBC na kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania, wakichezesha droo ya tatu ya kqampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo
ambapo wateja watano walijishindia pikipiki mpya aina ya Yamaha.
Meneja wa Kampeni ya Ibuka
Kidedea na NBC Malengo, Mtenya Cheya
(kushoto), akizungumza na mmoja washindi aliyeshinda zawadi ya bodaboda, huku
Meneja Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye (kushoto kwake) akishangilia katika
droo ya tatu ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto kwa
Dorothea ni; Meneja Chapa na Mawasiliano wa benki hiyo, David Raymond, Wakaguzi
kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga na Abdallah Hemedi
pamoja na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC)
imewahamasisha watanzania kutumia akaunti ya malengo ya benki hiyo kama
suluhisho ya changamoto mbalimbali za kifedha hivyo kuwawezesha kutimiza
malengo ya ndoto zao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo
kwenye droo ya tatu ya kampeni ya Ibuka kidedea na NBC Malengo, Meneja Chapa na
Mawasiliano wa benki hiyo, David Raymond alisema kwamba wateja wa benki hiyo waendelee
kutumia benki hiyo ili kutatua changamoto zao za kila siku.
“Huu ni mwanzo wa mwaka na watanzania
wengi wanakabiliwa na majukumu kadhaa kama vile ada za shule, kodi za nyumba na
bima za gari na nyumba, ni muhimu kwao kuendelea kuwa karibu na benki hii na
kwa wale ambao bado hawajafungua akaunti ya malengo ni vyema wakufungua ili
waweze kunufaika na zawadi,” alisema Raymond.
Meneja huyo wa Chapa na Mawasiliano
alisema kwamba droo hiyo ni ya tatu ambayo ilianza mwezi wa Oktoba mwaka jana
na washindi kadhaa wa bodaboda na safari za kutalii mbuga za wanyama Serengeti
na Visiwani shelisheli walikwenda na kurudi salama kwa usimamizi na ufadhili wa
benki hiyo kupitia kampeni ya malengo akaunti.
Kwenye droo hiyo ya jana washindi
watano waliibuka kidedea kwa kujishindia pikipiki aina ya Yamaha, washindi hao ni;
Luka Haule Baraka wa Dodoma, Juma Halfani kutoka Songea, Rebeka Ndosh anayeishi
Mwanza, Rosemary Kibodya wa Dar es Salaam na Restituta Mbuya wa Morogoro.
Kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC
Malengo itashuhudia washindi watatu wakiibuka kidedea na kujishindia zawadi ya
pikipiki ya miguu mitatu aina ya Toyo katika droo kubwa inayotarajiwa kufanyika
Mwezi Machi mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Absa Dar City Marathon 2024 zatimua vumbi jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga (kushoto), akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za nu...
No comments:
Post a Comment