Sunday, February 16, 2020

Absa Tanzania yawahakikishia wateja wake huduma bora zaidi
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Dr. Bernard Kibesse (katikati), akiinua glasi ili kuitakia
mafanikio bora benki ya Absa Tanzania akiwa pamoja na, kutoka kushoto;
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mkurugenzi Mtendaji
wa Kanda wa Absa, Saviour Chibiya, Mwenyekiti wa Bodi ya Absa Tanzania, Simon
Mponji na Mjumbe wa Bodi ya Absa Tanzania, DK. Suleiman Mohamed. Naibu Gavana
Kibesse alikuwa megni rasmi katika hafla iliyoandaliwa na Absa kwa wateja wake
jijini Dar es Salaama jana.
Benki Naibu Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse (kushoto), akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed alipoenda kuwa mgeni rasmi katika
hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini
Dar es Salaam jana ili kuwapa taarifa mbalimbali za utendaji wa benki
hiyo ambayo awali iliitwa Barclays Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Kanda wa Absa, Saviour Chibiya na Mwenyekiti wa Bodi ya Absa Tanzania, Simon
Mponji.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse (kushoto), akikaribishwa na Mwenyekiti wa
Bodi ya Absa Tanzania, Simon Mponji alipoenda kuwa mgeni rasmi katika
hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam
jana ili kuwapa taarifa mbalimbali za utendaji wa benki hiyo ambayo awali
iliitwa Barclays Tanzania.. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Absa wa Kanda,
Saviour Chibiya na Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse (wa nne kushoto), akigonganisha glasi na
wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania katika hafla waliyowaandalia wateja wao
jijini Dar es Salaam jana ili kuwapa taarifa mbalimbali za benki hiyo ambayo
awali iliitwa Barclays Tanzania. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi, Dk. Suleiman
Mohamed, Mkurugenzi wa Fedha, Obedi Laiser, Mwenyekiti wa Bodi, Simon Mponji na
Mkurugenzi Mtendaji, Abdi Mohamed.
Mkurugenzi Mtendaji wa Absa
Tanzania, Abdi Mohamed (wa pili kulia), akiwa na baadhi ya wateja wa benki hiyo
waliohudhuria hafla hiyo katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Absa
Tanzania, Abdi Mohamed (kulia), Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Absa Tanzana,
Aron Luhanga (katikati), pamoja na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa Absa
wakigonganisha glasi ili kutakiana afya bora pamoja na mafanikio ya benki hiyo
nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Absa
Tanzania, Abdi Mohamed, akigonganisha glasi na mmoja wa wakurugenzi wa benki
hiyo, Esther Maruma (kushoto), katika hafla hiyo. Kulia ni Naibu Gavana wa BoT,
Dk. Bernard Kibesse na Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda wa Absa, Saviour Chibiya.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Dk. Benard Kibesse akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na
Benki ya Absa Tanzania kwa ajili ya wateja wake na wadau wengine ili
kuwajulisha mikakati mbalimbali ya benki hiyo ambayo awali iliitwa Barclays
Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi
wa Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Selcom Tanzania, Sameer Hirji, mmoja wa waalikwa
waliohudhuria katika hafla hiyo katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam
jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Benki ya Absa ya endelea kusambaza upendo wa Siku ya Wapendanao kwa wajasiriamali
Meneja wa Masuala Endelevu na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi, akichagua maua, wakati baadhi ya wafanyakazi wa benki h...

No comments:
Post a Comment