MBUNGE MAVUNDE AGAWA VIFAA VYA KUJIKINGA NA COVID-19 KWA SHULE ZOTE ZA SEKONDARI JIJINI DODOMA. - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Tuesday, June 2, 2020

MBUNGE MAVUNDE AGAWA VIFAA VYA KUJIKINGA NA COVID-19 KWA SHULE ZOTE ZA SEKONDARI JIJINI DODOMA.


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amegawa vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19 kwa Shule zote za Sekondari za umma na binafsi zenye kidato cha Sita.

Mavunde amekabidhi leo vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Tsh 2,000,000 kwa wakuu wa Shule za Sekondari katika eneo la Jiji ya Dodoma ikiwa ni siku ya kwanza kwa wanafunzi wa kidato cha sita kurejea tena shuleni baada ya agizo la Mh Rais Dr John Pombe Magufuli kuhusu kufunguliwa tena kwa Vyuo na Shule.

"Baada ya Shule kufunguliwa tena nimeona kama Mbunge niunge mkono agizo la Mh Rais kwa kuhakikisha kwamba wanafunzi katika Jimbo langu wanasoma katika mazingira salama na ndio maana nimetoa majaba yenye uwezo wa kuhifadhi lita 1760,Sabuni lita 500,ndoo 50,sabuni boksi 25,Vitakasa mikono 500 na ndoo 50.

Rai yangu ni kuwataka wanafunzi wote wa kidato cha Sita kutumia muda huu kikamilifu kwa kusoma kwa bidii ili kufanya vizuri katika mitihani yenu ya mwisho ili kuendelea kulipaisha Jiji la Dodoma kwenye sekta ya Elimu"Alisema Mavunde

Akishukuru kwa niaba ya Wakuu wa Shule wa Sekondari,Mwl. Aloe Lyimo amemshukuru Mbunge Mavunde kwa msaada mkubwa uliokuja kwa wakati muafaka na kuahidi kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment

Absa Dar City Marathon 2024 donates hospital equipment to Mnazi Mmoja Hospital

Absa Bank Tanzania Head of Marketing and Corporate Affairs, Mr. Aron Luhanga hands over a part of hospital equipment to Mnazi Mmoja Hospital...

Pages