MCHIMBAJI MDOGO WA TANZANITE AIBUKA NA MAWE YENYE THAMANI YA SH. BILIONI 7.8. - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Wednesday, June 24, 2020

MCHIMBAJI MDOGO WA TANZANITE AIBUKA NA MAWE YENYE THAMANI YA SH. BILIONI 7.8.


Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite Bw. Saniniu Laizer  bilionea mpya Tanzania aliefanikiwa kupata Mawe mawili makubwa ya Tanzanite yenye dhamani ya Sh. Bilioni 7.8
Mawe makubwa mawili ya Tanzanite moja lina kilo 9.2 ambalo lina thamani ya shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.
Afisa Madini akionyesha moja ya jiwe la Tanzanite lilipatikana

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila amesema  kuwa leo Wizara inamtabua Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite Bw. Saninniu Laizer kuwa bilionea baada ya kupata  mawe makubwa mawili yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8.

Katibu Mkuu amesema kuwa mchimbaji huyo amepata mawe hayo mawili ambapo moja lina kilo 9.2 ambalo lina thamani ya shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.

"Na utofauti wake ni kwamba mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana kwenye machimbo ya tanzanite tangu machimbo yaanze na yamepatikana ndani ya ukuta wa Mirereni kwahiyo hii ni rekodi mpya ya kupata mawe yenye uzito huo" amesema Prof. Msanjila

Profesa Msanjila amesema kuwa sekta ya madini inauwezo wa kumfanya mtu kuwa bilionea kwa haraka, ameongeza kuwa kunahitaji kuwa uwekezaji wa dhati katika sekta hiyo.

No comments:

Post a Comment

Absa Bank Tanzania concludes Spend & Win campaign with great success, third Subaru Forester winner applauds service excellence

The final winner of Absa Bank Tanzania's three-month Spend & Win campaign, Ms. Amalia Lui Shio (center), receives the ignition key t...

Pages