KATIBU MKUU DKT. ALLAN KIJAZI AFANYA ZIARA FUPI EXPO 2020 DUBAI - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Sunday, November 28, 2021

KATIBU MKUU DKT. ALLAN KIJAZI AFANYA ZIARA FUPI EXPO 2020 DUBAI

 

Katibu Mkuu wa Wizara Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi ametembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai ambapo amepolekewa na Mkurugenzi wa Banda la Tanzania Bi. Getrude Ng’weshemi kutoka TanTrade na watumishi wengine kutoka Taasisi zinazoshiriki.

Dkt. Kijazi amepata fursa ya kufanya kikao kifupi na watumishi hao kutoka Taasisi zinazoshirki katika maonesho haya zikiwemo Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Eneo la Hifadhi la Ngorongoro (NCAA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ambapo amepokea taarifa ya maandalizi ya ushiriki wa Tanzania kwenye maonesho hayo, mafanikio yaliyopatikana na hatua zinazochukuliwa katika kuimarisha ushiriki wa uhakika wa Tanzania kwenye maonesho haya.

Aidha, Dkt Kijazi amesistiza maandalizi ya uhakika ya wiki ya Utalii yanayotarajiwa kufanyika tarehe 12 hadi 18 Desemba, 2021 pamoja na siku ya kitaifa ‘National Day’ itakayofanyika tarehe 26 Februari 2022. Maandalizi ya ushiriki katika programu ambazo zimeandaliwa yafanywe mapema kama ilivyopangwa na waratibu wa maonesho haya.

Amesema kuwa, "Fursa hii ya kushiriki kwenye maonesho haya ni ya kipekee na sisi kama Taifa tuna jukumu la kuitumia nafasi hii kuhakikisha Tanzania ina ushiriki wenye tija. Ninasisitiza Sekta zote zilizopata fursa ya kuwa sehemu ya maonesho haya ziendelee kuhamasisha ushiriki wa Tanzania hapa Expo 2020 Dubai hasa kwa Watanzania walio nyumbani ambao bado ushiriki wao ni mdogo. Naziasa Wizara, Taasisi na Sekta Binafsi kuwa kitu kimoja katika kuiwakilisha nchi na kuhamasisha ushiriki wa wadau mbalimbali wenye ushawisi katika jamii ili tulibebe jambo hili kwa pamoja kama taifa.

Vilevile, ametembelea banda la Tanzania ili kujionea jinsi nchi inavyotumia fursa hii kujitangaza kupitia sekta mbalimbali na inavyowavutia wawekezaji kupitia miradi mikubwa iliyopewa kipaumbele.

Banda lingine alilotembelea ni la Saudi Arabia ambapo lengo lilikua ni kuangalia, kujifunza na kuandaa vema ushiriki wa sekta ya utalii.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages