RC MAKALLA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUTORUDI NA KUFANYA BIASHARA KWENYE MAENEO WALIYOHAMA - Serious Business

Mgongopr.blogspot.com is a serious online platform of business and finance news from around Tanzania. We are a trusted site covering the entire spectrum, from small enterprises to large businesses entities. For photography, videography, media management, events management, advertising, public relations, translation, interpreters, and more services, please contact us: MPP Ltd phone: +255 767765454, email: mgongo@gmail.com

Breaking

Tuesday, November 2, 2021

RC MAKALLA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUTORUDI NA KUFANYA BIASHARA KWENYE MAENEO WALIYOHAMA

 
  • Asema Serikali itatumia sheria kuyalinda maeneo hayo na kurudi kufanya biashara katika maeneo hayo ni kosa.
  • Awataka Wamachinga wengi Wajitokeze kupata nafasi Machinga complex.
  • Atangaza nafasi 2,000 na route Za magari ya Kariakoo kufika machinga complex na masoko mengine mkoani  DSM.
  • Asema zoezi hili ni endelevu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Katika kuyalinda maeneo walipoondoka Machinga Serikali itatumia Sheria kwa Wote walioondoa Vibanda na kufanya Biashara Chini.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea Maeneo mbalimbali walipohamia Machinga kukagua changamoto ili Serikali izitatue, RC Makalla amewataka Wafanyabiashara waliokuwa Kariakoo, Karume, Msimbazi na Katika ya mji kufika Machinga Complex ili wapatiwe nafasi ambapo mpaka Sasa nafasi zilizosalia ni 2,100.
RC Makalla pia amewaelekeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuanza rasmi zoezi la Usafi kwenye maeneo yote walipoondoka Machinga na kuhakikisha yanalindwa yasivamiwe upya.

Aidha RC Makalla amesema Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zote zitakazoonekana kwenye maeneo walipopelekwa ili Biashara zifanyike na Wafanyabiashara wapate kipato.
Kwa mujibu wa sheria za miji na majiji zinaeleza kuwa kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa ni kosa kisheria ambapo adhabu kwa anaefanya kosa hilo ni kifungo Cha mwaka mmoja na faini ya Shilingi laki tatu.

No comments:

Post a Comment

Benki ya Absa Tanzania kuendelea kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu

Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto), Mwanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, Crispian ...

Pages